Rais Samia akutana na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 31 Oktoba, 2021 amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalumu wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika masuala ya biashara kati ya Uingereza na Tanzania Lord  John Walney.
Bw. Walney amekutana na Mhe. Rais Samia kujitambulisha akiwa na jukumu la kuwa kiungo kati ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji na utalii.

Amesema kukutana kwake na Mhe. Rais Samia kumempa fursa ya kujua vipaumbele vya Serikali ya Tanzania ambavyo vitamuwezesha kuwashawishi zaidi wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza katika sekta ya bishara na utalii nchini Tanzania 

Kwa upande wake Mhe. Rais Samia amemshukuru Bw. Walney kwa uamuzi wake wa kukutana nae na kujitambulisha kwake na kumueleza kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Uingereza katika kuchochea biashara baina ya nchi mbili hizo.

Mhe. Rais Samia amesema Serikali ya Uingereza na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa kibiashara kwa muda mrefu ambapo Uingereza ni moja kati ya nchi zinazoongoza kuwekeza nchini Tanzania, hivyo kupitia mjumbe huyo kutaongeza fursa zaidi za kibiashara katika kukuza ushirikiano wa uchumi na Uingereza.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad