Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Afariki..Ndio Mzungu wa Mwisho Kuiongoza Africa Kusini




FW de Klerk, rais wa zamani wa Afrika Kusini na mzungu wa mwisho kuiongoza nchi hiyo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85.


Bw de Klerk, ambaye pia alikuwa mhusika mkuu katika kipindi cha mpito cha taifa kuelekea demokrasia, alikuwa amepatikana na saratani mwaka huu, kulinagana na msemaji.



Bw de Klerk alikuwa mkuu wa nchi kati ya Septemba 1989 na Mei 1994.



Mwaka 1990 alitangaza kumwachilia huru kiongozi aliyepinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela, na kusababisha kura za vyama vingi mwaka 1994.



Taarifa kutoka kwa wakfu wa rais huyo wa zamani FW de Klerk siku ya Alhamisi asubuhi ilisoma: "Rais wa zamani FW de Klerk alifariki kwa amani nyumbani kwake Fresnaye (Cape Town) mapema leo asubuhi kufuatia mapambano yake dhidi ya saratani ya mesothelioma."



Taasisi hiyo ilikuwa imetangaza utambuzi huo - saratani inayoathiri utando wa mapafu - mwezi Juni mwaka huu.



FW de Klerk alikuwa amechukua nafasi ya PW Botha kama mkuu wa Chama cha National Party mnamo Februari 1989 na mwaka uliofuata akatangaza kuwa anaondoa marufuku ya vyama vilivyojumuisha chama cha Mandela cha African National Congress (ANC).



Vitendo vyake vilisaidia kukomesha enzi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, na akawa mmoja wa manaibu marais wawili baada ya uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1994 ambao ulishuhudia Bw Mandela akiwa rais.



Yeye na Mandela walishinda kwa pamoja Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 1993.



Hata hivyo, jukumu lake katika kipindi cha mpito kuelekea demokrasia lilipingwa sana. Mwaka jana, alijiingiza katika mzozo uliofanya ashtumiwe kwa kudharau uzito wa ubaguzi wa rangi. Baadaye aliomba radhi kwa "kubisha" juu ya suala hilo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad