Kauli ya mchekeshaji tokea pande za +254 (Kenya) @ericomondi aliyoitoa hivi karibuni kuhusiana na kiwanda cha burudani nchini Kenya imeonekana kuzua mjadala mkubwa mitandaoni nchini humo, Eric Omond alidai kiwanda cha sanaa ya Kenya kinakufa kwasababu ya uwingi wa matamasha ya wasanii tokea nje ya nchi hiyo wakati wasanii wazawa wanaishia kupiga show kwenye baa na mbaya zaidi wanakuwa wasindikizaji kwenye matamasha ya wasanii wageni na kuishia kulipwa pesa ndogo kabisa jambo linalopelekea sanaa ya Kenya kuchukuliwa cheap.
Kauli hiyo imewaibua wasanii kama mgenge @juacaligenge na @femi_one hit maker wa UTAWEZANA aliyemuattack Omond akimwambia kukaa Tanzania siku mbili amefunzwa sarakasi na kuanza kuwatusi wasanii wa Kenya huku akimtaka Omond kutofanya hivyo ili Heshima idumu.
Omond amemjibu Femi kwa kuanza kushangaa amepata wapi nguvu ya kumsemesha rais (President of Comedy Afrika) huku akimuuliza mara ya mwisho kufanya kitu cha maana kwenye muziki ni lini zaidi ya wimbo wake wa UTAWEZANA ambao pia ulikuwa wa @mejjagenge na @azz_iad ,pia akidai hatomjibu Jua Cali kwasababu ni Legend hivyo anamlindia Heshima yake.