Klabu ya Tottenham ya England imemtambulisha Antonio Conte kuwa kocha mkuu wa kikosi chao akiwa anakabidhiwa mikoba iliyoachwa na Nuno Espirito Santos kwa mkataba wa miezi 18, na inaripotiwa atapewa bilioni 471 za kitanzania kama pesa za usajili.
Kocha huyo zamani wa Chelsea alikuwa na wakati mzuri alipokuwa Stamford Bridge ambapo katika msimu wake wa kwanza alifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza na baadae kutwaa kombe la FA msimu uliofuatia.
Kwa sasa Conte atakuwa na kazi ya kuirejesha Spurs kwenye hali ya ushindani, baada ya timu hiyo kuvuna alama 15, katika michezo 10 wakiwa wamepoteza michezo mitano mengine ilipokuwa chini ya Nuno Santos.
Conte ambaye amekuwa na sifa za kutwaa mataji katika vilabu, hakuwa na kibarua baada ya kungátuka katika klabu ya Inter Milan ikiwa ni baada ya kuisaidia kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka takribani kumi na moja.