Hatimaye klabu ya Manchester United imefanya maamuzi ya kuachana na kocha wake Ole Gunnar Solskjaer baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha kushtukiza cha mabao 4-1, kwenye mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa jana Jumamosi.
Kwa mujibu wa Sky Sports, baada ya kipigo hicho cha kushtua, bodi ya Man United iliitisha kikao cha dharura kujadili hatima ya Solskjaer ambapo bodi hiyo ilifika makubaliano ya Solskjaer kutimuliwa kazi haraka iwezekanavyo.
Man United imefungwa mechi saba katika mechi 13 walizocheza msimu huu, rekodi mbovu chini ya kocha huyo raia wa Norway.