Ruby "Kusah Akiweka Mazingira Sawa Tutalea Wote Mtoto ila Kwa Sasa Hapana"



Msanii Hellen Majeshi maarufu kama Ruby a.k.a Mama Mchungaji ambaye kwasasa anatamba na goma lake jipya linaloitwa Jela, amefunguka kuwa hana bifu na mtu yeyote yule,wala hawezi kutana na mtu alafu akampita bila kumsalimia akidai kile kinachoendelea mitandaoni kwa hivi sasa kinaishia mitandaoni. Haya ameyazungumza wakati akifanyiwa mahojiano ndani ya kipindi cha EMPIRE ya EFM.

Hivi karibuni kumekuwa na hali ya kurushiana vijembe baina yake na Aunty Ezekiel ambaye yupo penzini na mzazi mwenzie na Ruby (Kusah),jambo ambalo limekuwa likitafsirika kuwa uwenda wakawa wanachukiana kweli.

Kingine Ruby amedai hajamzuia Kusah kulea mtoto wao bali ameangalia zaidi mazingira ambayo mtoto atalelewa,hivyo ameamua kubeba jukumu kama mama kuhakikisha mtoto anakuwa kwenye mazingira salama huku akidai ikiwa mzazi mwenzie, (Kusah) ataweka mazingira fresh basi atamruhusu walee wote mtoto. Ikumbukwe kwenye baadhi ya Interviews, Kusah amewahi kaliliwa kuwa ananyimwa haki ya kumlea mtoto bila sababu za msingi.

Kuhusu muziki wake, Ruby amedai anafikiria kuachia EP yake lakini pia ana ngoma nyingi kiasi kwamba anaweza achia hata Albamu,so mashabiki wake wakae mkao wa kula.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad