Ligi kuu ya NBC Tanzania inataraji kuendelea leo Oktoba 2, 2021 kwa michezo miwili ya mzunguko wa 5 ambapo Yanga itakuwa wenyeji wa Maafande wa Ruvu Shooting saa 12:15 jioni kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.
Kuelekea kwenye mchezo huo, Kocha msaidizi wa klabu ya Ruvu, Rajab Nakuchema amejinasibu kuwa, Ruvu wazee wa mpapaso ndiyo itakuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga kwa msimu huu wa mwaka 2021-2022.
“Sisi tutakuwa timu ya kwanza kufungua mlango wao. Tunaimani tutakuwa wa kwanza kuifungaYanga msimu huu” Alisema Rajab Nakuchema wakati anazungumza na wanahabari kwenye mahojiano kabla ya mchezo.
Upande mwingine, Kocha na Nahodha wa klabu ya Yanga hawakuweza kutokea kwenye mahojiano hao kwasababu ambazo mpaka sasa hazijatajwa na kufanyiwa changanuzi na bodi ya Ligi.
Mpaka sasa, Yanga imecheza michezo yake 4 na kupata ushindi kwenye michezo yote, ikifunga mabao 6, ikiwa haijaruhusu bao la kufungwa hata moja na kufikisha alama 12 ambazo zinamfanya awe kinara kwenye msimamo wa ligi.
Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>
Kwa Upande wa Ruvu Shooting, wenyewe wanashika nafasi ya 8 ikiwa na alama 6. Mchezo mwingine utakaochezzwa leo, ni Azam FC ambao watawakaribisha waima dhahabu kutoka mkoani Geita, timu ya Geita Gold saa 2:30 usiku, Chamazi