Rwanda yaanza kutumia pikipiki za umeme





Kwa miaka 12 Didier Ndabahariye amekuwa akiwasafirisha wateja wake katika barabara za mji wa Kigali -yeye ni mmoja wa maelfu ya wandesha piki piki za kibiashara, wanaofahamika kama motos.
Hivi karibuni aliachana na pikipiki yake ya kawaida na kugeukia ile ya umeme kuendesha shughuli zake katika mji mkuu wa Rwanda ikiwa ni moja ya piki piki za kwanza za umeme barani Afrika.

"Siku za kwanza, mambo hayakua mazuri kwa sababu nilikua sijazoea kuendesha e-motos na wakati mwingine piki piki inazima.

"Hata hivyo niliendelea na kazi, na baada ya siku chache nikajifunza mambo mengi kuhusu vile inavyofanya kazi na jinsi ya kuendesha. Ndipo nikaanza kupata pesa na kuweka akiba zaidi," Didier anaelezea.

Yeye ni mmoja wa waendesha piki piki 60 wa piki piki za umem kutoka kampuni ya Rwanda ya Ampersand.

"Sasa nazipenda pikipiki hizi - za umeme maarufu e-motokwani inauwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu bila kukumbwa na na matatizo ya kiufundi ukilinganisha na zile zilizo na injini - na inaenda vizuri, pia ni rahosi kuendesha."

Mradi huo wa kwanza wa kampuni ya Ampersand una malengo ya kuhakikisha piki piki zote nchini Rwanda zitakua za umeme katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kuna karibu piki piki 25,000 zinazohudumu kama teksi mjini Kigali,zingine zinaendeshwa kwa hadi saa 10, nahuwa zinasafiri mamaia ya kila mita kila sik.

"Pikipiki ni nyingi kuliko magari katika eneo hili la ulimwengu,"anasema Afisa Mkuu Mtendaji wa Ampersand Josh Whale.

"Injini zake ni rahisi na hazina aina ya teknolojia ya gharama kubwa ya kupunguza uzalishajiwa hewa chafu unayona kwenye magari ya kisasa. Pia zinaendeshwa kwa zaidi ya kilo mita 100 kwa siku, Hivyo basi kuchangia uchafuzi wa mazingira kutokana na uzalishaji wa hewa ya kaboni

Presentational grey line
"Nchi Rwanda, waendesha pikipiki wanatumia pesa nyingi kwa mwaka kugharamia petroli sawa na gharama ya kununua pikipiki mpya. Tumeonesha kuwa tunaweza kuleta njia mbadala ya kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuwapatia pikipiki zenye muundo sawa na zile walizo nazo sasa lakini kwa bei nafuu na utunzaji wake ni rahisi."

Ampersand inasema kupunguza gharama ya mafuta na utunzaji wa pikipiki kunaweza kumpatia mwedeshaji mapato mara mbili.

Kukiwa na wastani wa pikipiki milioni tano katika barabara za Afrika Mashariki, kunaweza kuwa na akiba kubwa katika utoaji wa CO2 ikiwa Ampersand na wasindani wake watachukua sehemu kubwa ya soko.

Ampersand nizaidi ya jukwaa la teknolojia. Inaunda pikipiki,beti zake na kuweka vituo vya kuchaji betri hizo.

Kila pikipiki inakaribu vipuri 150, ambazo zianunganishwa mjini Kigali. Cha muhimu ziadi ni kwamba betri zake zina muundo maalum na zimebuniwa na wahandisi wa Ampersand nchini Rwanda. Baadaye zinatengenezwa nje ya nchi na kurejeshwa nchini kuunganishwa na mafunsi wa ndani.

Kwa sasa Ampersand ina wafanyakazi 73 katika kiwanda chake cha kutengeneza pikipiki na wanahamia neo jipya mwezi huu uzalishaji unavyoendelea kukua.

Kapuni hiyo imeweka vituo vya ubadiliashia betri - ambapo wandesha piki piki wanaweza kubadilisha betri zilizoisha nguvu ili kupata zenye chaji - viruo vitano vinahudumu katika maeneo tofauti mjini Kigali.

Kila kituo cha kubadilishia betri kinagharimu karibu dola 5,000 za kimarekani (sawa na£3,700) kujenga - na kampuni hiyo inasema kuwa ina uwezo wa kujenga vituo 20 vya kubadilisha betri kwa gharama sawa na ya kujenga kituo kimoja cha petroli.

Serikali ya Rwanda ina jukumu kubwa katika mchakato wa kubadilisha mfumo wa usafiri kuwa wa kisasa, huku ikijaribu kutathmini faida na hasara ya uhamiaji huo wa kiteknolojia.

Kuna hofu ya kupoteza mapato ya kodi ya mafuta - lakini manufaa yake ni pamoja na kuhama kwa vyanzo vya nishati vinavyozalishwa nchini, kupunguza gharama za uagizaji wa mafuta kutoka nje na kuunda nafasi za kazi ikiwa pikipiki hizo zitaunganishiwa nchini humo.

Nchi hiyo imeanzisha mbinu kadhaa za kuwapa motisha watu wake kukumbatia usafiri wa kisasa.

Hii ni pamoja na ushuru uliopunguzwa wa umeme kwa vituo vya kuchaji betri na ardhi isiyolipishwa kwa ajili yao, maegesho maalum na njia za usafiri za magari yanayotumia umeme karibu na Kigali, na vikwazo vya utoaji wa hewa safi kwa magari yanayochafua mazingira.

Kampuni za usafiri zilipo nchi pia zinaonyesha nia ya kuchangia juhudi hizo.

Nchiin Rwanda, Volkswagen imekua ikifanya majaribio mradi wa ya usafiri wa kisasa tanngu 2019 kwa ushirikiano na na kampuni ya Siemens, ambayo imechangia kuanzishwa kwa Golfs 20 za umeme na vituo viwili vya kuchaji betri mjini Kigali.

Volkswagen inasema nchih iyo ina uwezo wa kuachana na injini za mwako na kuanza kutumia magari ya umeme.

"Kwa ushirikiano na wasirika wetu wa kimaendeleo Siemens na usaidizi kutoka kwa serikali ya Rwanda, Volkswagen inalenga kufanya mradi wa majaribio wa e-Golf kuwa mwongozo wa uhamaji wa magari ya umeme barani Afrika," anasema Andile Dlamini, wa Kundi la Volkswagen Afrika Kusini.

Kwa Ampersand, Rwanda imekuwa hatua ya kwanza tu barani Afrika, na kampuni hiyo kwa sasa inazinduliwa katika nchi jirani ya Kenya na nchi zingine muda mfupi baadaye.

Ingawa kuna changamoto za kusambaza magari ya umeme kote Afŕika - kama vile uhaba wa ujuzi maalum, kutosita kwa wawekezaji wa mitaji na kuvurugika kwa minyororo ya ugavi - Bw Whale anasema kuwa bara hilo linaweza kuwa kinara katika mabadiliko ya kimataifa ya uchukuzi wa magari ya kisasa.

Kiwango cha mtaji unaojhitajika sio "rahisi kupatikana", anasema, na huenda ukatolewa na serikali za kimataifa ili kuharakisha mchakato huo.

"Tunatumai tunaweza kuonyesha kwamba wakati wa kukumbatia mfumo wausafiri wa kutumia umeme umewadia - kwa kila mtu - na usafiri bila kuchafua mazingira safi sio kitu ambacho tunatakiwa kuona kikifanyika katika chi zilizoendelea, kwani ulimwengu unaelekea huko miongo kadhaa kutoka sasa. Badala yake nchi masikini zinaweza kukumbatia teknolojia hii ya gharama nafuu inayofadhiliwa na wakati wa kuwekeza ni - sasa."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad