Serikali yatoa Msimamo wake GSM Kudhamini Timu zaidi ya Moja




Dar es Salaam. Serikali hatimaye imetoa msimamo wake kuhusu kampuni ya GSM kudhamini timu zaidi ya moja na kueleza kuwa hilo wanawaachia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuwa ndio inaangalia sheria.

Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni GSM kutangaza kuzidhamini timu za Pamba na Coastal Unioni ya Jijini Tanga, ukiachilia mbali kuwa bado wanawadhamini Yanga SC.

Kutokana na hilo wadau mbalimbali wa mpira wa miguu wamekuwa na mtazamo tofauti huku wengine wakihofia huenda GSM ikaingilia katika kupanga matokeo.

Hata hivyo leo Jumamosi Novemba 6, 2021, Mwanaspoti walitaka kusikia kwa upande wa serikali inalizungumziaje suala hilo na akitolea ufafanuzi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa, amesema hawaoni kama lina shida endapo sheria zitafuatwa.

"Ukiachilia mbali TFF pia tuna baraza la Michezo (BMT) ambalo lipo karibu katika kusimamia sheria hizo, hivyo sioni na wala wananchi wasiwe na shaka katika hilo kwani kama kutatokea ukiukwaji wowote hawatasita kuchukua hatua kwa muhusika" amesema Waziri huyo.

Pia Bashungwa amesema katika suala hilo la udhamini wa GSM watu wasitie shaka nalo kwa kuwa kama ni sheria za mpira zipo, hivyo endapo kutaonekana kuwa na mambo tofauti wahusika watawajibishwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad