Shahidi aeleza kutowatambua watu kwenye CCTV kamera kesi ya Sabaya

Arusha. Shahidi wa nane katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, Johnson Kisaka, ameieleza Mahakama kuwa hawezi kuwatambua na kuwaelezea watu wanaoonekana kwenye video za CCTV, alizowasilisha mahakamani hapo.

Shahidi huyo wa Jamhuri ni Ofisa uchunguzi wa maabara ya uchunguzi wa kielektroniki kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Makao Makuu.

Alidai mahakamani hapo kuwa video hizo za Benki ya CRDB Arusha tawi la Kwa Mromboo za Januari 22, mwaka huu alizichukua Mei 31, mwaka huu.

Alitoa ushahidi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, alipohojiwa na Wakili wa utetezi, Mosses Mahuna, mbele ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo.

Shahidi huyo alidai kuwa aliagizwa kwenda kufanya uchunguzi wa taarifa za video zilizorekodiwa kwa CCTV kamera kwenye benki hiyo na ampatie Ramadhan Juma (Ofisa Takukuru) kwa ajili ya uchunguzi na ndiye ataweza kuelezea zaidi juu ya wanaoonekana.

Alidai katika video hizo sita aliona watu wakiingia na kupata huduma za kifedha katika benki, lakini jukumu lake halikuwa kuchunguza watu wanaoonekana, bali kuchukua video hizo na kuandaa ripoti ya namna alivyozichukua na kuziwasilisha kwa mchunguzi pasipo kuingiliwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad