BAADA ya mapumziko ya weekend, leo Jumatatu, Novemba 8,2021 kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu inaendelea.
Mbowe na wenzake wanashtakiwa kwa tuhuma za ugaidi, kesi inayoendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam.
Katika mwendelezo huo, upande wa mashtaka unatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi na Mahakama inatarajiwa kupokea ushahidi wa shahidi wa nane kati ya mashahidi 24.
Shahidi wa mwisho kabla ya leo (wa saba) alikuwa Inspekta Mahita Omar Mahita, aliyetoa ushahidi wake Ijumaa iliyopita. Inspekta Mahita alikuwa miongoni mwa kikosi cha maofisa wa Polisi kutoka Arusha kilichowatia mbaroni washtakiwa wawili katika kesi hiyo.
Kulingana na aina ya ushahidi wake, kiongozi wa jopo la mawakili wa utetezi, Peter Kibatala alitumia saa 2:25 kumhoji maswali mbalimbali shahidi huyo kuhusiana na ushahidi wake, muda ambao ni mrefu zaidi kutumiwa na wakili mmoja kumhoji shahidi tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa Septemba 15, mwaka huu.
Wakili Kibatala alilieleza Mwananchi kuwa alitumia muda mwingi zaidi kumhoji shahidi huyo kuliko mashahidi wengine kutokana na ushahidi wake ambao alisema uligusa maeneo mengi.
Alieleza mashahidi wengine ambao itakapofika zamu yao kutoa ushahidi atatumia muda mwingi kuwabana kwa maswali ni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jumanne na Koplo Goodluck, ambao pia walikuwa katika timu hiyo iliyowatia mbaroni watuhumiwa, pamoja na Luteni Denis Leo Urio.
Luteni Urio ni Ofisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), kutoka kikosi Maalum (Special Force) au 92 KJ yaani kikosi cha makomandoo, kilichoko Ngerengere eneo la Sangasanga mkoani Morogoro.
Huyu ni shahidi katika kesi hiyo, kwani mujibu wa maelezo ya maandishi ya mashahidi wa upande wa mashtaka, ndiye anadaiwa kuhusika kuibua tuhuma zinazowakabili washtakiwa.
Wakati kesi hiyo ikisubiriwa kuendelea leo, swali na ama shauku ya wadaawa, hususan washtakiwa na mawakili wao pamoja na wadau wanaofuatilia kesi hiyo ni kujua ni nani shahidi wa nane na kusikia ni ushahidi gani atakaoutoa.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfan Hassan, Adamu Hassan Kasekwa maarufu kama Adamoo na Mohamed Abdillahi Ling’wenya.
Washtakiwa hao watatu walikuwa askari wa JWTZ, 92 KJ, Ngerengere ambao waliachishwa kwa sababu za kinidhamu.
Jaji ameingia
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa
WS Robert Kidando anasimama
Jaji: Ndiyo
Robert Kidando anatambulisha Jopo la mawakili wa serikali
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Pius Hilla
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige
Ignasi Mwinuka
Wote wanawakilisha Jamhuri katika kesi hii..
Wakili Peter Kibatala nae anasimama na anatambulisha Jopo la mawakili wa upande utetezi..
Maria Mushi
Evaresta Kisanga
Hadija Aron
Alex Massaba
Idd Msawanga
Seleman Matauka
Dickson Matata
Nashon Nkungu
Fredrick Kihwelo
John Mallya
Peter Kibatala
WS: Shauri hili lina kuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna Shahidi Mmoja, Tupo tayari Kuendelea
Kibatala: Tupo tayari Mheshimiwa Jaji
WS: Mmoja anaenda Kumfuata Shahidi
JAJI yupo Kimyaaaa anaandika Kidogo
Peter Kibatala anaomba Radhi kwa Kuchelewa Kidogo
Jaji: Shahidi wa ngapi huyo?
WS: Shahidi wa 8
Jaji: Majina yako
Shahidi: Superitendent Jumanne Malangahe
Jaji: Umri
Shahidi: 46
Jaji: Kabila
Shahidi: Msukuma
Jaji: Shughuli yako
Shahidi: Afisa wa Polisi
Jaji: Dini yako
Shahidi: muislam
Shahidi: Wallah wabillah taala nathibitisha kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie
WS: Kitambulisho Bwa Jummane Unafanya Kazi gani
Shahidi: Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha
WS: Majukumu yako ni nini
Shahidi: Kuzuia uhalifu
Kukamata Uhalifu
Kupeleleza Makosa ya Jinai
Kuwaongoza Askari Waliochini yangu ktk Shughuli ya Upelelezi
WS: Ukiwa Mkuu Wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru, Je Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha Mwaka 2020 alikuwa ni nani
Shahidi: Alikuwa afande ACP Ramadhan Kingai
WS: Katika Majukumu yako ya Upelelezi na Kusimamia Askari waliopo Chini yako no Shughuli gani katika Upelelezi hufanyika
Shahidi: Baada ya Shauri Kufunguliwa, ndipo Upelelezi Unapoanza kwa kuwakamata wa husika, Kupelele Shauri na
Kukagua eneo la Tukio
Pamoja na Kuku Sanya Vielelezo namambo Mengine kutokana Aina ya tukio
Wakili wa Serikali: Elezea hapa Mahakamani Tarehe 04 Mwezi August 2020 ulikuwa wapi
Shahidi: 04 August 2020 nilikuwepo katika Kituo Changu cha Kazi, Upelelezi Wilaya ya Arumeru, Nikiwa Ofisni Kwangu nilipigiwa Simu na Afande Kingai, Akinitaarifu kuna Safari Ni jiandae Ya Kwenda Kufanya Moshi, Mkoani Kilimanjaro
WS: ilikuwa Muda gani wakati anakupigia Simu
Shahidi: Ilikuwa Muda wa Saa 12 na Kitu
WS: ya Muda gani
Shahidi: Ya Jioni
WS: Nini kiliendelea Kutokana na alichokutaarifu
Shahidi: Nilijiandaa na Saa 1 kasoro aliwasili nikiwa Ndani nikasikia Muungurumo wa Gari, nikampokea na Kwenda Ofisini Kwangu Kisha tukaketi
WS: Wakati Kingai anafika, Yeye alikuwa na nani
Shahidi: Alifika na Askari Jumla walikuwa watano akiwemo yeye Mwenyewe, Insp Mahita,
Detective Coplo Francis, Detective Coplo Goodluck pamoja na Dereva wa Gari Detective Constable Azizi
WS: Wakati Kingai anaingia Ofisini Kwako hawa wenyewe walikuwa wapi
Shahidi: Wali ingia Wote Ofisini Kwangu
WS: Elezea sasa baada ya Kuingia Ofisini nini Kiliendelea
Shahidi: Afande Kingai Alianza Kutoa Taarifa Kwamba Kipo Kikundi Cha Kihalifu ambacho kinatarajia Kufanya Matukio ya Kihalifu hapa Nchini
Ambayo ni Kulipua Vituo Vya Kuzuia Mafuta, Kuanzisha Vurugu na Maandamano, Kukata Miti na Magogo na Kuyaweka katika Barabara Kuzia Magari
Kupita pamoja na Kuwadhuru Viongozi wa Serikali Akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole sabaya
Na Kwamba Baadhi yao walikuwa wana wawasili Moshi Mkoani Kilimanjaro, na Kwamba Kikundi hicho kinaratibiwa na Freeman Aikael Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Na hivyo Miongoni Mwa Wahalifu hao watatu walikuwa wameshawasili Moshi kwa ajili ya kutekeleza Uhalifu huo
Akasema Jukumu letu ni Kuzuia Uhalifu huo Kutendeka na Kuhakikisha Wahalifu hao tunawakamata
Baada ya Kumalizia a kutoa Maelekezo hayo ilikuwa ni Takribani saa Moja
Tukianza Safari ya Kuelekea Moshi
WS: Pale Moshi Mlifika Saa ngapi
Shahidi: Saa 2 Usiku
Shahidi: Afande Kingai akasema anaendelea Kupokea Taarifa Kutoka kwa Msiri wake Kutoka Kwa Msiri wake
WS: Elezea Sasa Kesho yake Asubuhi nini Kiliendelea
Shahidi Tulikutana Kituo cha Mjini Kati pale Moshi akasema, Tuendelee Kupokea Taarifa Mpaka atakapojiridhissha Mazingira Yamekaaje
Shahidi Tuliendelea Kuwepo Maeneo yake Mpaka Takribani Saa 6 Mchana Afande Kingai akatuita tena
Akatuambia amepata Taarifa wale Wahalifu Wapo Maeneo ya RAU Madukani, Walikuwa watatu na akatuelekeza Mwonekano wao na aina ya Nguo walizo vaa.