Soma Kisa Cha Mtoto Huyu Akiwa Kabeba Mwili wa Mdogo Wake Alifariki Kwa Njaa Vita ya Pili ya Dunia



Picha hii ilichukuliwa wakati wa vita vya pili vya dunia (World War II) mwaka 1945. Kijana mdogo wa Kijapani alisimama mbele ya makaburi akiwa amebeba mwili wa mdogo wake aliyefariki kwa kukosa chakula kutokana na wazazi wao kuuawa kwenye vita.

Mtoto huyu alisimama muda mrefu akiwa anasubiri mwili wa mdogo wake uchomwe moto kisha aondoke kwenda kuona namna mpya ya kuishi kwa upweke na maisha bila baba wala mama katika umri mdogo.

Hakuwa na ndugu yeyote aliyemtegemea kwa sababu ndugu zake wote waliuawa katika vita hivyo. Alikua anaenda kuanza maisha yake katika ulimwengu wa peke yake wenye giza totoro.

Mwandishi mmoja wa TNYT aliwahi kusimulia kisa cha mtoto huyo na kusema "Mvulana huyo alikuwa amefunga mdomo kwa kuung'ata kwa nguvu kubwa mpaka damu zilikuwa zikichuruzika toka pembeni mwa mdomo wa chini aliokuwa ameung'ata ili kujizuia kulia. Damu zilipochuruzika sana alifuta kwa mkono na kuendelea kung'ata.

Askari mmoja aliyekua makaburini hapo akamuomba mwili huo akisema "Nipe mzigo ulioubeba mgongoni, tukauchome moto" Kijana akamjibu "Sio mzigo, ni mdogo wangu mpendwa, amefariki"

Kutokana na taratibu za ibada za mazishi za Kijapan ni kuchoma mwili moto, kijana alimkabidhi mwili askari huyo na kuondoka akiwa ameng'ata mdomo na kukunja sura. Alikua na maumivu ya aina mbili. Maumivu yaliyotokana na majeraha ya kung'ata mdomo na maumivu ya kupoteza ndugu zake na wazazi wake katika vita hiyo. Maumivu ya kwanza yalikua ishara ya kuvumilia maumivu ya pili.

Mpaka leo huko Japan, picha hii hutumika kama ishara na uvumilivu mtu anapopatwa au kufikwa na matatizo makubwa.

Umejifunza nini?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad