Sri Lanka: Genge Linalochukua Picha za ngono Kuwatapeli Pesa Watu




Wanaume wawili wanashikiliwa na polisi ya eneo la Akkaraipattu nchini Sri Lanka kwa madai ya kuzungumza na wanaume kwa simu na kuchukua picha zao za utupu bila kujua.



Polisi inasema mmoja wa wanawake alikuwa ni mama mjane mwenye watoto watatu na mwingine alikuwa ni mwanaume aliyekuwa ameoa. Wakati walipowasilishwa mahakamani hakimu aliagiza waendelee kuwekwa mahabusu kwa siku 14.



Wanaume hao waliweza kuiba rupia laki tatu za Sri Lanka kutoka kwa mwanaume aliyepigwa picha za utupu na mwanamke, walimwambia aweke pesa hizo mahali fulani na wakajaribu kuzichukua , lakini walikamatwa na polisi waliokuwa wamejificha mahali hapo.



Muathiriwa tayari amepoteza laki sita rupia za Sri Lanka kutokana na mwanamke huyo.



Mwanamke huyo aliwasiliana na wanaume kwa njia ya simu ya mkononi bila kuonesha uso wake hadi mwisho wa mazungumzo hadi kuwafanya wavue nguo zao katika picha simu ya video ya ngono, na kuirekodi kwenye simu yake ya mkononi.



Polisi baadaye waliiambia Idhaa ya BBC Tamil kwamba mwanamke huyo amekuwa akipokea pesa nyingi kwa kutunza picha hizo za ngono.



Wakati huo huo, BBC Tamil imebaini kuwa picha za utupu za baadhi ya maafisa wa ngazi ya juu zilipatikana kwenye simu ya mwanamke aliyekamatwa na polisi.



Hatahivyo, hakuna taarifa zilizotolewa na polisi hadi sasa juu ya iwapo mwanamke huyo pia aliwalazimisha wao pia kutoa pesa.



Mwanaume mwingine na mwanamke wamekamatwa kwa kuwa na uhusiano na genge hilo.



Kwa mujibu wa BBC Tamil, watu hao wawili waliokamatwa walikuwa na uhusiano wa kifamilia na mjomba na mkwe wa na walijifanya kuwa mume na mke na kuwanyang'anya pesa waathiriwa.



Walitishia kwamba watatunza picha: Waathiriwa walikiri

Washukiwa walikamatwa baada ya malalamiko yaliyowasilishwa kwenye kituo cha polisi cha Akkaraipattu na mwanaume mmoja ambaye alikuwa tayari ameibiwa rupia laki 6 pesa taslimu na genge hilo.



Akizungumza na BBC Tamil kuhusu jinsi alivyoibiwa mwanaume huyo alisema:



"Miaka mitatu iliyopita nilipokea simu ya rafiki yangu kutoka akaunti ya facebook anayeitwa Fatima Shipani. Nikaipokea. Nilisajiri simu yangu katika Facebook . Siku moja mwanamke mmoja alizungumza nami na kujitambulisha kama 'Sanas'."



"Msichana yule alizungumza nami lugha chafu. Wakati mmoja nikaanza kuzungumza hivyo sawa na yeye. Mazungumzo yale yalikuwa ya ukaribu sana kiasi kwamba aliniita 'wewe'."



"Siku moja aliniomba anitazame nikiwa mtupu.



Nilionekana mbele ya kamera ya 'video ya simu' nikiwa na nguo ya ndani. Lakini hakuwahi kuonesha uso wake . "



"Siku chache baada ya hili kutokea mwanamke mwingine alizungumza nami. Alikuwa rafiki wa mwanamke mwingine ambaye tulikuwa tumezungumza naye kabla- alijitambulisha.



Aliniambia kuwa anapicha zangu nikionekana nimevaa nguo ya ndani. Halafu akaanza kuniongelesha lugha chafu; Pia mimi nikaanza kuzungumza kama yeye."



"Mwanamke alijyeongea nami mwara ya mwisho Septemba 18 alinipigia simu kwa simu yake ya mkononi na akaniambia kwamba anahitaji rupia laki tano za dharura na akanitaka nimpatie. Akasema pia kwamba angerejesha pesa hiyo mwezi Disemba. Nilisema sikuwa na pesa nyingi kiasi kile ."



"Mwanamke aliyezungumza nami mara ya kwanza aliniambia kuhusu hilo. Alisema rafiki yake aliiba picha zangu za video nilizokuwa nimevaa nguo ya ndani kutoka kwenye simu yake na akaniambia nimpe pesa anazo niomba. Nilisema siwezi."



"Mwanamke niliyezungumza naye mara ya pili alitishia kutuma picha zangu kwenye mtandao wa kijamii kama sijalipa pesa anazotaka. Niliogopa sana filamu hiyo ingetolewa jinsi ilivyo. Kwahiyo nililazimika kuchangisha pesa ili nisipoteze utu wangu. Kwahiyo nilifanya kazi ngumu sana kuchangisha pesa ."



"Mwanamke niliyezungumza naye mara ya pili tarehe 23 Septemba aliniambia niache pesa laki tano (rupia) saa moja asubuhi katika eneo la Oluvil - Qatar. Nilifanya kama alivyonieleza.



Wiki mbili baadaye nilipokea simu kutoka kwa mwanamke niliyezungumza naye mara ya pili tena. Alitaka nimnunulie simu ya mkononi, alinitaka nimpe rupia elfu 40.



Pia aliniambia nitume pesa kwa njia ya mfumo wa utumaji pesa kwa njia ya simu 'eZ cash' na niache nguo yangu ya ndani mahala alipotaka niiache. "



Wiki mbili baadaye, wanamke wa pili alisema mume wake amerejea kutoka Ulaya.



Mwanamke aliyezungumza nami mara ya kwanza, akaniomba tena nimtumie rupia elfu 10, nikatuma.



Siku moja mwanaume mmoja akanipigia simu kwenye simu yangu ya mkononi akajitambulisha kama mume wa mwanamke niliyezungumza naye mara ya pili. Alinitishia kuwa nimemuharibu mke wake na anakwenda polisi. Niliogopa sana. Wakati mmoja niliogopa ninaweza kupata mshituko wa moyo.



Nilimwambia asiende polisi niko tayari kufanya chochote atakachoniambia. Alisema anaenda Japan na anahitaji rupia laki tano . Nilisema nitampa. Hatahivyo sikuwa na pesa. Ilikuwa inatisha. Nikutana na nikamwambia kilichonitokea. Alinipeleka kwa mwanasiasa mwenye mamlaka makubwa na nikamwambia suala langu.



Mwanasiasa alinipeleka katika kituo cha polisi cha Akkaraipattu tarehe 28.



Niliwaambia kila kitu kilichotokea pale. Kulikuwa na mpango wa kuwakamata wahusika wa genge, "alisema muathiriwa huyo.



Je walikamatwa vipi?



Tarehe 29 mwezi uliopita, mtu mmoja alilalamika katika kituo cha polisi Akkaraipattu. Washuiwa walikuwa tayari wamemwambia aweke pesa walizokuwa wamemtaka awape katika eneo moja la Oluvil, Qatar saa moja asubuhi.



Polisi waliamua kufanya hivyo pia. Lakini badala ya pesa, waliweka rundo la karatasi mahali hapo.



Saa moja usiku, muathiriwa aliweka ''kifurushi'' hicho kwenye eneo hilo.



Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Akkaraipattu waliwasili mapema katika eneo hilo wakiwa wamevaa mavazi ya kawaida, wakawasubiri huku wakiwa wamejificha karibu naeneo hilo.



Muathiriwa aliwasiliana na mtu ambayer alimwambia aache pesa kweney simu. Akamwambia aliweka tayari pesa katika eneo alilomwambia awali.



Walimwambia muathiriwa aondoke mara moja kwenye eneo hilo na aende eneo la Nintavur , lililopo kilomita 10, na 'awaambie alipo' kwa njia ya simu ya mkononi ili kuhakikisha hajasimama pale. Alifanya kama alivyoagizwa.



Maelezo ya polisi kuhusu kilichotoea eneo la tukio

"Tulikuwa tumejificha gizani. Ilikuwa saa moja na nusu usiku. Piipiki ikapita eneo zilipokuwa zimewekwa pes ana kwenda kwenda moja kwa moja barabarani. Mara moja tukamzingira. Alikuwa ni mwanamke. Aliyekuwa anaendesha pikipiki ni mwanaume. Tumemkamata pia. "



Muathiriwa ameiambia BBC kuwa mahabusu aliyekamatwa alikuwa na sauti ya mwanamke ambaye alizungumza naye mara ya pili.



Simu ya mkononi iliyokamatwa na polisi kutoka kwa mwanamke aliyekamatwa ina picha za utupu za wanaume kadhaa.



Inasemekana zinajumuisha picha za baadhi ya maafisa wa nazi ya juu wa serikali katika wilaya ya Ampara pamoja na wanasiasa na viongozi wa kidini.



Kulingana na polisi, genge hilo limekuwa likichukua picha za wanaume na kuwaingiza katika video za ngono(ponografia) kwa zaidi ya miaka minane.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad