Stanislav Petrov: Mtu ambaye Aliokoa Dunia




Miaka 30 iliopita , tarehe 26 mwezi Septemba 1983 , dunia iliokolewa kutokana na uwezekano wa bomu la kinyuklia. Mapema siku hiyo Kulikuwa na Ving'ora vilivyoashiria kwamba kulikuwa na shambulio la kombora kutoka kwa Marekani .


Uchunguzi wa kompyuta ulibaini kwamba makombora kadhaa yalikuwa yamerushwa . Itifaki ya jeshi la Usovieti ilikuwa kujibu kombora la kinyuklia na kombora jingine la kinyuklia.

Huu ulikuwa wakati ambapo mishipa ya mtu ilikuwa inakaribia kapasuka, kulingana na mwana wa Luteni Stanislav Petrov -mwanamume aliyezuia uwezekano wa vita vya kinyuklia mwaka 1983.

Dmitry Petrov anasema kwamba babake alikuwa katika mahala muhimu wakati mwafaka.
Anasema kwama babake ambaye alikuwa Luteni kanali wa vikosi vya angani vya Usovieti alihudumu huko serpukhov-15, kambi ya Usovieti iliyotambua onyo la kwanza la kurushwa kombora la masafa marefu

Anasimulia kwamba usiku wa Septemba 26 mwaka 1983, Petrov alichukua nafasi ya mwenzake wakati wa zamu ya usiku.

Lakini dakika kumi na tano baada ya usiku wa manane alisikia king'ora kikilia, asijue kwamba onyo lake iwapo lisingeangaziwa lingeangamiza dunia

King'ora hicho kilionya kuwa Marekani ilikuwa imerusha kombora. Kwasababu halikuwa jambo la kawaida alilazimika kukagua huduma zote, labda iwapo kumetokea hitilafu ya kimitambo

Luteni huyo kama inavyosimuliwa na mwanawe aliamini zaidi huduma za kuona kwa macho

Yeye na wenzake waliokuwa zamu siku hiyo walifanya uchunguzi wa kufuatilia kwa njia ya setlaiti lakini hawakufanikiwa kuliona kombora hilo.

Kwanini hawakufanikiwa kuliona kombora hilo?

Wakati huo ilikuwa vigumu kuliona kombora hilo kwa njia ya setlati kwasababu jua lilikuwa linatua.

Vilevile kulikuwa na mstari wa terminator , mstari uliopo kati ya mchana na usiku, mbali na kwamba pia setlaiti yenyewe ilikuwa katika mstari huo

Petrov alikuwa na muda wa chini ya saa moja kuamua iwapo kombora lilirushwa au la anasimulia mwanawe

Wakati huo uhusiano kati ya Marekani na Usovieti uliwa na misukosuko. Mzozo huo ulihusu kile kilichofahamika kama Euromissiles.

Uliendelea mwishoni mwa miaka ya 1970 na kufikia kilele chake mwaka 1983.

Wakati huo wote Muungano wa Usovieti ulikuwa unaboresha makombora yake ya masafa ya kati, ambapo makombora mapya yalikuwa yachukue sehemu ya yale ya zamani.

Hatua hii ilisababisha malalamishi makubwa kutoka nchi za magharibi.

Ili kujibu hatua hiyo, Marekani ilifanya mpango wa kupeleka makombora mawili hatari Magharibi mwa Ulaya, kombora la Pershing II na lile la kurushwa kutoka ardhini.

Na mwaka 1983 ndio wakati makombora haya yalikuwa yanawasili Ulaya

Katika hali tete kama hiyo, uamuzi mbaya ungetosha kuzua hali ambayo ingesababisha kutokea vita vya nuklia.
King'ora hicho kililia mara kadha kuashiria kurushwa kwa makombora mengine.

Mfumo huo ukaonyesha hali ya juu ya kutegemewa.


Petrov alihitajika kuripoti kwa kamanda wa cheo cha juu na alijua kuwa iwapo angethibitisha kwamba Marekani ilikuwa imerusha kombora ,Usovieti nayo ingejibu

Ilikuwa kazi yake kufanya maamuzi. Alikuwa tayari amefunzwa kwa hilo

Uamuzi wake uliookoa dunia

Baba yangu alikuwa na muda mgumu kwa sababu kurushwa kombora moja haitakuwa ni kutangaza vita bali hatua hiyo ingesababisha misururu kadhaa ya mashambulizi.


Hakuamini kuwa kungetokea vita kabisa, kwa sababu hakungekuwa na washindi.


Kwa hivyo alichukua simu na kusema kuwa mfumo ulikuwa unatoa habari zisizo za ukweli.

Huu ulikuwa ukiukaji mkubwa wa maagizo anayofaa kufuata . Kitu muhimu ambacho angepaswa kufanya ilikuwa kupitisha ujumbe huo kwa mkubwa wake. Lakini ndio uamuzi ambao uliokoa dunia.

''Nilikuwa na data zote kubaini kwamba kulikuwa na shambulio . iwapo ningetuma ripoti yangu kwa mkubwa wangu , hakuna mtu angeiping''a, alinukuliwa na BBC Urusi miaka 30 baada ya usiku huo wa kihistoria.

Bwana Petrov - ambaye alistaafu wadhfa wa Luteni kanali kabla ya kifo chake alikuwa miongoni mwa maafisa waliopokea mafunzo ya kiwango cha juu ambao walihudumu katika mojawapo ya vitengo vya jeshi la Usovieti la kutoa tahadhari za mapema .

Uchunguzi uliofanywa ulionyesha kuwa setilaiti ilikuwa imechanganyikiwa na miale ya jua iliyorudi kutoka kwa mawingu.

Mwaka 1984, Petrov alistaafu na kuhamia Fyrazino mji mdogo nje ya Moscow.

Habari za kisa hicho zilikuja kuibuka miaka 15 baadaye, mwaka 1998.


Hakuzungumza kuhusu kisa hicho, hakutaka kukumbuka kabisa kwa sababu hakuchanganyikiwa na hali hiyo isiyo ya kawaida.

Mtu mwingine, katika hali kama hiyo, anaweza kuthibitisha kuwa kombora limerushwa na ni hivyo.

Baada ya habari hiyo kuibuka, Petrov alitembelewa na vyombo vya habari, na akaanza kupokea barua kutoka kwa watu kote duniani.
Hata kama anwani yake wakati mwingine haikujulikana. Hakukuwa na anwani ya posta, namba ya simu, fax au hata barua pepe.

Karl Schumacher raia wa Ujerumani alimtembelea Petrov mwaka 1998.

Na akaniambie niingie na kisha tukaketi kwenye meza ya jikoni.

Nilikuwa ninataka nimjue na nilitaka nimshukuru.


Urafiki wao ukadumu kwa karibu miaka 20.

Petrov akatambuliwa kimataifa na kupewa tuzo.

Alijivunia uamuzi wake mzuri.

Kwa sababu kile alichokuwa anafikiri kwa ile nusu saa katika kituo kile ni 'lazima nifanye uamuzi, lakini utakuwa uamuzi wa kweli?'
Na alitaka awe sahihi.


Stanislav Petrov alifariki Mei mwaka 2017.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad