Taarifa kuhusu Clatous Chama kutoka kwa Watu wake wa karibu sana ni kuwa yupo katika hatua za mwisho za kuvunja mkataba na RS Berkane (Mutual Agreements)
🔉Kabla ya Chama kuanza mazungumzo ya kuvunja mkataba aliwasiliana na Simba pekee, kuulizia uwezekano wa yeye kurejea nchini
🔉Simba walibariki hilo ila waliweka wazi kuwa hawana pesa za kuvunja mkataba wake na Berkane hivyo suala hilo lipo juu yake kulimaliza, Chama aliridhia hilo
🔉Mpaka kufikia leo hii, Chama na wakala wake wapo zaidi ya 90% ya kukamilisha uvunjaji wa mkataba kwa maslahi ya pande zote mbili na atakuwa huru
🔉Tayari Simba wamemfungulia milango na kuandaa mshahara na marupu rupu yaleyale kama alivyoondoka, ikiwemo kodi ya nyumba Mikocheni, Dar Es Salaam
🔉Mpango rasmi ni yeye kuwasili nchini mapema zaidi na huenda kabla hata ya derby ya Kariakoo (kama kila kitu kitakuwa sawa) kukamilisha mkataba wake, huku akianza kucheza mwezi January
⛔Kama Simba itafuzu hatua ya makundi Shirikisho basi ataorodheshwa kwenye list kwa ajili ya michuano ya Kimataifa
⛔Watu wake wa karibu wanasema Chama anaitazama Simba pekee, akitumia neno "In Tanzania, it's only Simba"
♻️Mwamba wa Lusaka to Simba for the last dance IS ALMOST A DONE DEAL