TMA "Wananchi zingatieni utabiri wetu"




WANANCHI wametakiwa kuzingatia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) ili waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Akizungumza katika Mjadala wa Kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia ya Nchi na athari zake uliofanyika kwa njia ya Mtandao , Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dkt Agness Kijazi amesema upo uhusiano wa moja kwa moja wa mabadiliko ya tabia ya nchi na utabiri wanaoutoa.

"Mifumo ya hali ya hewa kama wananchi wakiichukulia kwa jinsi walivyozoea kulingana na mabadiliko haya yaliyopo wataenda ambavyo sivyo, ukijua kwamba mvua zitaanza kipindi fulani na kuisha kipindi fulani pasipo kuangalia sayansi hii iliyopo na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo na tabia ya nchi duniani utakuta kwamba unakwenda siyo sawa kwa hiyo kuna uhusiano mkubwa kati ya mabadiliko ya tabia ya nchi na utabiri tunaoutoa " amesema Dkt.Kijazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad