Ishu ya @travisscott imeendelea kuchukua headlines baada ya tamasha lake la Astroworld Fest lililofanyika usiku wa tarehe 5/11 huko Houston Marekani, kusababisha vifo vya watu 8 na majeruhi kibao.
Ukiachana na ufafanuzi wa @lawyerforworkers kwenye hiyo clip, Baadhi ya watu wameendelea kumshambulia Travis Scott kuwa anapaswa kufunguliwa mashtaka ya mauaji maana hata watu walipoanza kudondoka wengine mbele yake hakusimamisha show na akaendelea kutumbuiza tu kitu ambacho kimechukuliwa kama ni makusudi hadi pale maafisa wa polisi walipotumia nguvu.
Kingine kinachomuweka kwenye wakati mgumu ni ishu yake ya mwaka 2015 alipokamatwa kwasababu ya kuhamasisha watu kugomea ulinzi uliokuwa ukisimamia utaratibu wa tamasha la Lollapalooza alilokuwa akiperform kwa kuwahamasisha kuruka vizuizi vilivyowekwa na kupanda jukwaani.
2017 pia Travis Scott alikamatwa kwa kuhatarisha usalama wa umati kwenye show yake kinyume na maelekezo yaliyowekwa. Ni mara nyingi msanii huyo amekuwa akionywa kwa vitendo vyake vya kuhamasisha vurugu kwenye show zake ila ni kama sikio la kufa.