Uganda: Watu zaidi ya ishirini wakamatwa baada ya mashambulio Kampala




Siku ya Alhamisi, Novemba 18, siku mbili baada ya mashambulizi mawili yaligharimu maisha ya watu wanne mjini Kampala, polisi ya Uganda inasema imewaua kwa risasi washukiwa watano wa kundi la waasi la ADF, Allied Democratic Forces. Washukiwa 21 pia wanazuiliwa na idara ya usalama kote nchini.


Polisi ya Uganda ilifanya ilielezea kuhusu uchunguzi wake siku ya Alhamisi, siku mbili baada ya mashambulizi mawili ya kujitoa muhanga  mjini Kampala. Mashambulizi yaliyodaiwa na kundi la Islamic State lakini polisi wa eneo hilo wanashuku kundi la waasi la wa Uganda la ADF kuwa lilihusika na mashambulizi hayo.



Washukiwa wanne wa kundi la ADF wameripotiwa kuuawa katika majibizano ya risasi katika eneo la Ntoroko, magharibi mwa nchi hiyo, karibu na mpaka wa DRC. Mshukiwa wa tano alisemekana kuuawa kwa kupigwa risasi nje kidogo ya jiji la Kampala alipokuwa akijaribu kutoroka kukamatwa kwake: alikuwa kiongozi wa Kiislamu ambaye alikuwa na jukumu katika kuwarejesha waasi wa ADF katika mji mkuu wa Kampala.



Operesheni ya polisi katika kipindi cha siku mbili zilizopita pia ulipelekea kukamatwa kwa washukiwa 21, kulingana na msemaji wa vikosi vya usalama nchini Uganda.



Hatimaye watu 13 wakiwemo wanawake sita na watoto wameripotiwa kukamatwa katika eneo la Ntoroko, Magharibi mwa nchi hiyo ambako kuna matawi ya kundi la ADF linaendesha harakati zake kwa miaka 25  upande wa pili wa mpakani nchini DRC. , na ambaye hivi karibuni lilijiunga na kundi la Islamic State.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad