Uganda yakamata washukiwa wa ugaidi huku engine 7 wakiuwawa




Uganda inasema kwamba washukiwa saba wameuwawa na wengine 106 wanashikiliwa kutokana na matukio ya kigaidi. Hayo yametokea wakati wa oparesheni iliyofanywa na vikosi vya usalama wakihusishwa na washukiwa watatu wa mabomu ya kujitoa muhanga katika mji mkuu Kampala wiki iliyopita, kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Reuters ya Jumatatu. 

Kundi la Islamic State ambalo lina ushirikiano na kundi la uasi la Uganda la Allied Democratic Forces (ADF) limedai kuhusika na shambulizi la Nov 16, ambalo limeuwa watu saba ikijumuisha watu watatu waliojitoa muhanga, na kujeruhi dazeni zaidi. Afisa mmoja wa polisi alikuwa miongoni mwa wengine wanne waliofariki dunia na kati ya watu 37 waliojeruhiwa 27 walikuwa ni maafisa wa polisi. Polisi haukutoa taarifa za kina za namna ya washukiwa hao saba walivyo uliwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad