Umeisikia hii ya MO kumrejesha Chama Simba SC ?




Uongozi wa klabu ya Simba umegusia suala la kumrejesha kiungo wake wa zamani Clatous Chama aliyetimkia  kwenye klabu ya RS Berkaine ya Morocco dirisha kubwa lililopita na kuwapa Simba mafanikio makubwa.
Uwezekano wa Chama kurejea Simba unazungumzwa baada ya Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba, Abdallah Salim Mhene ‘Try Again’ kuwathibitishia wanasimba kuwa wanapesa za kutosha hata kumrejesha Chama.

"Simba Oyeee! Oyee! MO bado yupo sana. Na yeye ameniambia mzigo upo wa usajili. Awe nani sijui nani atatinga. Sijui Chama sijui nani sijui nani. Ameniomba niwafikishie salama, anawasalimia sana anawapenda sana". Amesema Try Again.

Hayo yamesemwa mchana wa leo wakati Try Again alipokuwa anaongea mbele ya wanasimba waliojitokeza kwenye mkutano wa mkuu wa mwaka 2021 uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwl Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Taarifa hizo pia huenda zitawapa nguvu wanasimba kwani walipigwa na butwaa zito waliposikia fununu za watani wao wa jadi Yanga kuhusishwa naye.


 
Chama aliichezea Simba kwa misimu mitatu na kufanikiwa kubeba makombe matatu ya Ligi Kuu na matatu ya FA huku wakifika hatua ya robo fainali mara mbili katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad