Umeme kukatika wachangia mitambo ya maji kuungua




Imeelezwa kuwa kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, unasababisha wananchi wa maeneo mengi kukosa huduma ya maji kutokana na mitambo ya kusukuma maji kuungua jambo linalotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka ili kuondoa kero hiyo.


Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Mijini na Vijijini (RUWASA) wilaya ya Bariadi, Herry Magoti, ameiambia Jumuiya ya Watumiaji wa Maji wilayani hapa kuwa, mitambo ya kusukuma maji imekuwa ikiunguzwa kutokana na umeme kukatika mara kwa mara, hali inayosababisha jamii kukosa maji kwa wakati.



Kulingana na hali hiyo, mamlaka ya wilaya ya Bariadi imekiri kuwapo kwa changamoto ya umeme, ingawaje serikali imejielekeza kujenga kituo cha kupoza umeme mkoani humo ili kuondoa vikwazo hivyo kwa jamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad