Unaambiwa Bei za Mabando Tanzania Zinaua Mziki wa Bongoa


Katika dunia ya sasa, views ni kipengere mojawapo muhimu sana cha kuitrendisha sanaa ya nchi fulani katika uso wa dunia.

Hali imekua tete baada ya mabando kupanda bei saizi youtube watu wanaingia kwa machale.

Views chache pia zinawapunguzia mapato wasanii, youtube wanalipa kwa kigezo kinachoitwa CPM (Cost Per Mile) kipimo chao ni malipo kwa kila views 1,000. kwa hapa kwetu wastani huwa ni wa dola 1 hadi dola 1.5 (shilingi elf 2,300 hadi shilingi 3,500) kwa views 1,000 na malipo huwa yanafanyika kila tarehe 22 au 23 kupitia western union ama kupitia bank (wire transfer)

Ilishazoeleka msanii kuandaa fungu la milioni 3 au zaidi kwajili ya video, hii yote ilitokana na uhakika wa kurudisha pesa hio kwa views , lakini kwa sasa kwa hii hali wasanii watakosa pesa za kurekodi videos zeye ubora wa hali ya juu na pia hata huko studio wataanza kujibana, hii kitu itakata mabawa wa sanaa yatu ambayo ilianza safari ya kusambaa nje ya nchi,

Video ya "bia tamu" ilisubiriwa kwa hamu lakini cha kushangaza imefikisha views mil 1 baada ya siku tatu.

Video ya "Bwana mdogo" ya Alikiba FT patoranking imefikisha views mil 1 kwa mbinde sana , wakati hapo awali Alikiba alikuwa na moto mzito, Views Mil 1 chap chap. Hii sio kwa Alikiba na Marioo tu bali ni kwa kila msanii, hivi sasa kupata views sio mchezo kabisa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad