Unaambiwa Vunja Bei Hapokei Simu ya Aristote, Kauli Siku ya Harusi ilikwama



Kwa mujibu wa Mwijaku ni kuwa baada ya Harusi ya chawa maarufu mjini,Aristote kumalizika, Aristote amekuwa ni mtu wa kumpigia simu mwenyekiti wa kamati, bwana Fred Vunja Bei na simu zake hazipokelewi.

Hii imekuja kutokana na kauli ya Aristote Baada ya Diamond kuanza kutunza harusini hapo, Aristote alidai atunzapo Diamond hakuna mwingine mwenye uwezo wa kutunza, kauli ambayo iliwakata stimu hadi waliofanya harusi yake ing'are, akiwemo mwenyekiti wa kamati,Vunjabei aliyekodisha hadi Helicopta na timu yake nzima ya Too Much Money😁

Sasa unaambiwa Honeymoon ilikuwa apelekwe nje ya nchi kwa udhamini wa Vunja bei ila mpango huo umeshakufa ,Honeymoon itafanyika Bonyokwa😁. Haya kayasema Mwijaku ndani ya Leo Tena ya Clouds Fm.

Hii inaitwa Boss akinuna, Chawa uweweseka😁

By Sójamedia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad