Siku kadhaa nyuma,kulikuwa na maneno kuwa msanii Diamond Platnumz na Uncle Shamte haziivi na wametimuana huko Madale, Hii ilitokana na breki ya kutopostiana kwenye mitandao ya kijamii kati ya Mama Dangote na Uncle Shamte kama walivyowazoesha waja hapo kabla.
Hasa hii leo tarehe 22/11 Mbele ya camera za Refresh ya Wasafi TV, Uncle Shamte amedai hakumuoa Mama Dangote ili waje kuachana na pia dhana ya kuwa Uncle analelewa ife maana yeye ndiye anamlea Mama Dangote na ndio maana anajidekea.
Kingine Uncle amedai mtoto wake, Diamond ana mijengo kama 67 hivi maana kwa miaka mitano waliyokaa pamoja, Uncle Shamte kasimamia ujenzi wa mijengo 31.