Ushahidi wa Inspekta Maulid kesi ya kina Mbowe huu hapa




Shahidi wa nne wa upande wa mashtaka katika kesi ndogo ndani ya kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo ametoa ushahidi katika Mahakama Kuu ya Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.


Kesi hiyo ndogo inatokana na mshtakiwa wa tatu Mohamed Ling’wenya kupinga maelezo ya onyo yaliyotolewa na shahidi wa nane katika kesi ya msingi, SP Jumanne, akidai hakuwahi kufikishwa Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam ila alilazimishwa kusaini maelezo ambayo hakuyatoa.



Inspekta Issa Maulid anaapa kwaajili ya kuanza kutoa ushahidi



Anaongozwa na wakili wa Serikali Robert Kidando



Wakili Kidando: Unafanya kazi gani



Shahidi: Ni askari polisi



ADVERTISEMENT



Wakili: Unazifanyia wapi?



Shahidi: Nazifanyia Kikosi cha Polisi Tazara Dar es Salaam.



Wakili: Umesema uko Kikosi cha Reli Tazara, kikosi chako cha kazi ni kipi?



Shahidi: Pugu road na sasa ni Kaimu mkuu wa kituo cha Pugu



Shahidi: Majukumu haya nilikabidhiwa toka tarehe 3/6/2021 na majukumu yangu ni kusimamia askari ninaowaongoza na kusimamia majuku yangu ikiwemo kusimamia askari kutimiza majukumu waliyopewa



Shahidi: Jukumu lingine ni kusimamia doria, mali za Serikali yakiwemo majengo magari samani na silaha na mali zingine zote.



Shahdi: Jukumu la nne ni kushughulikia malalamiko yote yanayofikishwa kituoni ikiwemo kufungua kesi kupeleleza na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa, kusimamia mahabusu walioko kituoni kujua hali zao za kiafya, kuhakikisha wamepata huduma za chakula kwa wakati.



Shahidi: Kila inapofika asubuhi nakagua mahabusu na kukagua kitabu cha kumbukumbu za mahabusu (DR) nikiwa nimeongozana na askari wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume.



Shahidi: Baada ya kufika mahabusu naanza kuita jina moja baada ya lingine. Baada ya kumuita namuhoji kosa tarehe aliyoingia nalinganisha na yaliyoandikwa kwenye kitabu.



Shahidi: Dhumuni la kuwahoji ni Ili kufahamu kilichaoandikwa kwenye kitabu na kujiridhisha kisha narudi kwenye chumba cha mashtaka na kusaini kitabu.



Shahidi: Malengo ya kufanya ukaguzi ni kuainisha taarifa na idadi ya mahabusu, pia kufanya upelelezi na kukamilisha endapo upelelezi utakuwa umekamilika naamuru washtakiwa wapelekwe mahakamani.



Shahidi: Kama ukaguzi bado ukamilishwe kwa wakati na endapo mtuhumiwa ana haki ya kupewa dhama adhaminiwe



Shahidi: Tazara najihusisha na makosa yote ya jinai yanayotokea, Maeneo yote (within compound) katika station zake, karakana zake na ofisi zake.



Shahidi: Mpaka sasa nina miaka 17 Tazara



Wakili wa Serikali: Ongeza sauti



Shahidi: Kuanzi Mei 10, 2020 nilikuwa operation officer wa Kikosi cha Tazara kuanzia Dar es Salaam hadi Tunduma



Shahidi: Majukumu yangu makubwa yalikuwa ni kupata taarifa za mahabusu walioko kwenye vituo vyote na kutoa taarifa, kusimamia mazoezi ya utayari kwa askari wote ,



Shahidi: Agost 2,2020 nlipewa barua ya kukaimu Mkuu wa kituo cha Tazara baada ya aliyekuwepo kwenda likizo ya siku 20



Shahidi: Kuanzia Agosti 3 hadi Septemba 6, 2020 nilikaimu nafasi hiyo ambapo mkuu wa Kituo Richard Obutu aliiacha.



Shahidi: Majukumu niliyokuwa nayo ni kusimamia nidhamu.



Shahidi: Katika Majukumu yangu kuna kitabu cha kufungulia taarifa, kitabu cha kuandika kumbukumbu za mahabusu (DR) na kitabu cha kunakili mali anazokutwa nazo mtuhumiwa baada ya kufanya upekuzi.



Shahidi: Nakumbuka Agost 7,2020 nilifanya ukaguzi kama inavyopaswa katika mahabusu hapakuwa na mtuhumiwa hata mmoja



Shahidi: Agosti 8,2020 nilifanya ukaguzi alikuwepo mtuhumiwa mmoja mwanaume aliyekuwa mtumishi wa Serikali



Shahidi: Agosti 9,2020 palikuwa na watuhumiwa wawili, wanafunzi wa kiume ambao walikuwa wanatuhumiwa kuhatarisha miundo mbinu ya Reli, tuliwakamata wakifungua nati za Reli.



Wakili wa Serikali: Ulibaini vipi hao watuhumiwa?



Shahidi: Kama ilivyo kawaida inapofika asubuhi napitia Detention Register na katika ukaguzi nilijiridhisha mahabusu hao wapo.



Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kufanya Shughuli hiyo ya Ukaguzi wa Mahabusu, wewe unauthibitisho gani kama watuhumiwa hao walikuwepo



Shahidi: Udhibitisho wangu mkubwa katika ukaguzi ni kitabu cha kumbukumbu za mahabusu (DR). Kipindi ambacho na Kaimu kitabu hicho kilikuwa kinatunzwa charge room



Shahidi: Niliendelea kukaimu hadi Septemba 6,2020 aliporudi Richard Obutu



Shahidi: Nimkabidhi mali kama nilivyoorodhesha silaha,magari, samani, mahabusu waliokuwepo na nyaraka za siri za Serikali. Vitabu vilivyokuwa vinatumika ikiwemo DR havikuingia kwenye makabidhiano vilibaki CRO



Wakili Kidando: Ulikaimu tena nafasi hiyo kutoka kwa nani?



Shahidi: Kwa Richard Obutu ambaye amehamishiwa Zanzibar.



Wakili: Kwanini ulikabidhiwa majukumu hayo?



Shahidi: Baada ya SP Richard Obutu kuhamishwa.



Wakili: Makabidhiano hayo yalifanyikaje?



Shahidi: Kwa nyaraka



Wakili: Ulikabidhiwa nini?



Shahidi: Magari, silaha nyaraka za siri, na  vitabu vingine mbalimbali ikiwemo DR



Wakili: DR ulizokabidhiwa zipi?



Shahidi: Miongoni mwa DR nilizokabidhi ni pamoja na zilizotumika ambazo nimezihifadhi.



Shahidi: Novemba 14 alikuja mtu kutoka ofisi ya DI aliyejitambulisha Inspekta Swilla, nikiwa ofisini kwangu, nikaambiwa naitwa chini.



Shahidi: Baada ya kuonana nae alinihoji kuhusu DR iliyotumika Agosti 7,8,9 , 2020 na kunieleza kuwa inahitajika mahakamani kwa ajili ya kutolea ushahidi. DR hiyo ilikuwa imetumika na kuisha tangu Machi 2021 kwa hiyo hazikuwepo CRO.



Shahidi: Baada ya kuondoka nilirudi na kuitafuta nilipoikagua nikakuta Agost 7,2020 hapakuwa na mahabusu, Agosti 8,2020 palikuwa na mmoja na Agosti 9 palikuwa na wawili.



Wakili wa Serikali: Kuna kesi ipo hapa Mahakamani hebu niambie kama kuna majina ya Halfan Bwire Hassan na Adam Kasekwa.



Shahidi: Kupitia DR ya tarehe hizo washtakiwa waliopo mahakamani hawakuwepo.



Wakili: Mheshimiwa Jaji tunaomba kumkabidhi Shahidi kielelezo kwaajili ya utambuzi?



Wakili: Hiyo ni nini?



Shahidi: DR ya Pugu road



Wakili: Umeitambuaje?



Shahidi: Kwa maandishi yaliyoko nje



Wakili: Utakitambuaje?



Shahidi: WEF01 Januari 1/2019. Ndani kuna kumbukumbu namba zilizoandikwa kwa kifupi



Wakili: Unataka Mahakama ifanye nini?



Shahidi: Ipokee kama kielelezo



Baada ya mawakili wa utetezi kupitia kitabu cha kumbukumbu ya mahabusu (DR ) Wakili wa mshtakiwa wa kwanza, wa pili, wa tatu na wanne hawana pingamizi.



Jaji: Napokea  kama kielelezo p3 kwenye Kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya upande wa mashitaka



Kielelezo kimepokewa na mahakama kielelezo namba tatu cha upande wa mashtaka katika kesi ndogo.



Wakili wa Serikali: Kitabu hicho kilitumika kuanzia lini hadi lini



Shahidi: Kuanzia 01.01.2019 Mpaka 29 May 2021



Wakili wa Serikali Kidando amemaliza.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad