Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani imetenga fedha kwaajili ya kuwapeleka watafiti wa miamba katika kijiji cha Mfuru kata ya Marumbo wilayani humo, lengo likiwa ni kuchukua sampuli ya mawe makubwa mawili yanayodhaniwa kuwa ni vimondo ili kubaini kama ni vimondo halisi.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Hanan Bafagih amesema hatua hiyo imekuja kufuatia hoja iliyoibuliwa na madiwani wakiomba kupelekwa wataalam kwaajili ya kupima mawe hayo ambayo huenda yakawa vyanzo vya utalii na hivyo kuongeza mapato kwa halmashauri hiyo.