Polisi wa mpakani nchini Uholanzi wanasema wamewakamata wanandoa ambao walikuwa wametoroka hoteli ya karantini karibu na uwanja wa ndege wa Schipol huko Amsterdam.
Maafisa walisema mmoja wao amekuwa akijitenga baada ya kukutwa na virusi vya corona baada ya kusafiri kutoka kutoka Afrika Kusini.
Wenzi hao walifanikiwa kupanda ndege kuelekea Uhispania lakini walikamatwa kabla tu ya kupaa.