Wafanyakazi wa Manowari ya Marekani iliyoanguka wafukuzwa kazi




 Jeshi la wanamaji la Marekani limewafukuza wafanyakazi wa ngazi za ya juu watatu waliokuwa kwenye manowari ya nyuklia iliyoanguka kwenye mlima ulio chini ya maji.


Kamanda wa Cameron Aljilani na wengine wawili waliondolewa baada ya uchunguzi wa tukio hilo katika bahari ya Kusini ya China.



Manowari hiyo ya Marekani ilikwama mwezi uliopita, ikafanya chombo hicho kuelea juu kwa wiki.



Maafisa wa jeshi la wanamaji wanasema wahudumu hao "wangeweza kuzuia" mgongano huo.



Wiki iliyopita, jeshi la wanamaji lilisema manowari hiyo iligonga "mlima wa bahari" usiojulikana wakati wakifanya doria.



Mabaharia kumi na tano walipata majeraha kidogo. Manowari hiyo kwa sasa inaangaliwa ikiwa imeharibika huko Guam katika Bahari ya Pasifiki kabla ya kurejea Washington kufanyiwa matengenezo.



Tukio hilo lilitokea huku eneo hilo likiwa na mvutano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad