Wakenya Watakiwa Kutumia njia Mbadala, Wakati Huu Kondomu zikiadimika




Serikali ya Kenya imewataka wakenya kutumia njia mbadala wakati huu ikihangaika kukabiliana na uhaba wa kondomu.


Taifa hilo linadaiwa kuwa na upungufu mkubwa wa kondomu, takwimu zikionyesha kwamba kondomu zinazohitajika ni milioni 455 kwa mwaka tofauti na milioni 1.6 zinazotolewa na serikali kwa sasa.



Kwa mujibu wa gazeti la Star Kenya, taarifa kutoka mfuko wa kimataifa wa kupambana na Ukimwi, TB na Malaria (Global Fund), inaonyesha kwamba zaidi ya kondomu milioni 20 zilisambazwa mwaka jana nchini humo.



Gazeti hilo limemnukuu katibu mkuu wa wizara ya afya ya nchi hiyo, Mercy Mwangangi akisema serikali ya nchi hiyo itafanya kila linalowezekana kukabiliana na upungufu wa kondomu.



Maswali ni mengi mitandaoni kuhusu hizo njia mbadala, kwa sababu kazi ya kondomu ni kuzuia maambukizi ya magonjwa na mimba. Licha ya kutozitaja moja kwa moja, moja ya njia mbadala inayofahamika zaidi ni kuacha kabisa kushiriki tendo la ndoa kama njia ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ama mimba zisizotarajiwa.



Inaelezwa kwamba upungufu huo unatokana na tozo kubwa inayotozwa na saerikali kwenye baadhi ya bidhaa zikiwemo zilizotolewa kama misaada, huku wahisani wengine wakilazimika kuelekeza misaada yao kwenye nchi zingine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad