Watu 6 wamethibitika kufariki dunia mpaka sasa huku wawili kati yao wakiwa maafisa polisi, kufuatia milipuko miwili kutokea jijini Kampala nchini Uganda karibu na Bunge na kituo cha Polisi katikati mwa jiji, leo Jumanne, Novemba 16, 2021.
Watu wengine 33 wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali za karibu kwa ajili ya matibabu na uhakiki wa waliojeruhiwa ukiendelea kufanyika ili kujua idadi.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa bomu jingine limekutwa karibu na Transifoma katika jengo la Kooki Tower na mengine mawili yamekutwa karibu na barabra ya Buganda ambapo yote yalitenguliwa huku Kitengo cha Polisi cha kupambana na ugaidi kikiendelea kutafuta mabomu mengine zaidi kama yapo ili kuyategua.