Watekaji wa Haiti wawaachilia wamishonari wawili kati ya 17





Watu wawili miongoni mwa wamishonari 17 wa Marekani na Canada waliotekwa na genge nchini Haiti mwezi uliopita wameachiliwa, maafisa wa misaada wamesema.


Kanisa la Christian Aid Ministries alisema Jumapili kwamba watu hao wawili walikuwa "salama, wenye furaha, na walitunzwa vyema".



"Hatuwezi kutoa au kuthibitisha majina ya wale waliotolewa yaliyotangazwa," kanisa lilisema, bila kutoa taarifa zaidi.



Taarifa ya kutekwa nyara kwa wamishonari na familia zao, wakiwemo watoto, iliripotiwa tarehe 16 Oktoba.



Walikuwa wamerejea kutoka katika safari ya kuwatembelea mayatima wakati basi lao lilipotekwa na wajumbe wa genge katika mji wa Ganthier, mashariki mwa mji mkuu, Port-au-Prince.



Wote waliotekwa wakati huo-wanaume watano, wanawake saba na watoto watano- raia wa Marekani, isipokuwammoja ambaye alikuwa ni raia wa Canada.

Genge hilo lililoripotiwa kupanga utekeji huo, kwa jina 400 Mazowo, baadaye lilidai kikombozi cha dola milioni moja(£740,000) kwa kila mmoja wa mateka hao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad