Watu 61 wapatikana na virusi katika ndege iliyotoka Afrika kusini kwenda Uholanzi




Watu sitini na mmoja waliowasili mjini Amsterdam katika ndege mbili zilizotoka Afrika Kusini wamepatikana na virusi Covid-19, Dwamesema maafisa wa Uholanzi.

Wamewekwa katika eneo la kujitenga katika hospitali iliyopo karibu na uwanja wa ndege wa Schiphol.

Walikuwa ni miongoni mwa wasafiri wapatao 600 walikuwa wameshikiliwa kwa saa kadhaa baada ya kuwasili huku wakipimwa virusi.

Maafisa wa Uhonzi wanafanya vipimo zaidi kuangalia iwapo kuna visa vovyote vya kirusi kipya cha Omicron, kilichopewa jina hilo Ijumaa, kilichotajwa kama aina mpya ya kuhofia na WHO.


Ni Waafrika Kusini wapatao 24% tu ambao wamepata chanjo kamili hadi sasa

Aina hiyo mpya ya kirusi cha covid kwa mara ya kwanza kiliripotiwa kwa Shirika la afya duniani nchini Afrika Kusini tarehe 24 Disemba.

Wakati huo huo Uholanzi ni mojawapo yan chi kadhaa za Muungano wa Ulaya zinazohangaika kudhibiti rekodi ya idadi ya maambukizi.

Katika kipindi cha saa kadhaa nchi nyingi kote duniani zimeweka masharti ya kusafiri kutoka katika nchi za kusini mwa Afrika zilizoathiriwa.

Nini tunachokifahamu mpaka sasa kuhusu Kirusi hicho?
Kirusi hicho kinaitwa B.1.1.529 na huenda Ijumaa hii Shirika la Afya Duniani (WHO) likakipa kirusi hicho jina la Kigiriki (kama lilivyo kwa kirusi cha Alpha na Delta).

Prof Tulio de Oliveira, mkurugenzi wa Kituo cha Kukabiliana na Magonjwa ya mlipuko nchini Afrika Kusini, alisema kulikuwa na "mfululizo usio wa kawaida wa mabadiliko" na kwamba ilikuwa "tofauti sana" na tofauti aina zingine za virusi ambazo zimeenea.

"Aina hiki cha kirusi kilitushangaza, kina mabadiliko mengi zaidi kuliko ambavyo tulitarajia," alisema.

Profesa Richard Lessells, kutoka Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini, alisema: "Tunapata wasiwasi kwamba virusi hivi vinaweza kujiimarisha, na kuimarisha uwezo wake kuenea kutoka kwa mtu hadi mtu, lakini pia kinaweza kuepuka mfumo wa kinga."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad