Wawili Wasimamishwa Kazi Kwa Kufanya Mapenzi Wodini

 


Siku chache baada ya mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Kaliua, Irene Apina kusimamishwa kazi kwa tuhuma za kukataa kumpa matibabu mtoto wa miaka mitano, wauguzi wawili wa hospitali hiyo wamesimamishwa kazi kwa vitendo vya utovu wa nidhamu.

Watumishi hao, mmoja anatuhumiwa kufanya mapenzi wodini na daktari ambeye yupo katika mafunzo kwa vitendo huku mwingine akituhumiwa kuwa kinara katika utoaji wa mimba.

Katika kikao chake na watumishi wa sekta ya afya, Mkuu wa Wilaya ya Kaliua (DC), Paul Chacha aliwasimamisha kazi watumishi hao na kila mmoja kumpa tuhuma zake.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Novemba 29, 2021 DC Chacha amesema kuwa baada ya kuwasimamishwa kazi, tayari kuna timu imeundwa kuchunguza tuhuma zao

Amesema kuwa muuguzi wa afya katika hospitali hiyo ambaye jina limehifadhiwa anatuhumiwa kwa kuwa kinara wa utoaji mimba huku mhudumu wa afya akilalamikiwa na wagonjwa kufanya mapenzi wodini na daktari ambaye yupo kwenye mafunzo

"Kama huyu mtu ni daktari akiwa mafunzoni maana yake ndio kipindi cha matazamio halafu bado mnamuacha hapo anafanya nini? Taarifa yake iende mbaya kuwa hafai" amesema Mkuu huyo wa Wilay

Daktari huyo aliye mafunzoni anatuhumiwa kufanya mapenzi wodini ambapo inadaiwa wagonjwa wamekuwa wakikerwa na kitendo hicho na kuanza kulalamika.

Mkuu huyo wa wilaya amesema hataki kuona mambo yasiyofaa katika Wilaya anayoiongoza na kwamba hatasita kuchukua hatua stahiki lengo ni kukomesha tabia mbaya na watumishi wawe mfano kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad