Waziri Anyoosha Mikono Afrika Kusini ni Taifa Hatari Sana"




Takwimu za hivi karibuni za uhalifu nchini Afrika Kusini "zinashtua sawa na robo ya takwimu iliyopita", Waziri wa Polisi Bheki Cele amesema wakati akiwasilisha takwimu hizo.


Kwa mujibu wa akaunti ya serikali ya Twitter, alisema kuwa takwimu za kipindi kati ya Julai na Septemba mwaka huu zinaonesha kuwa Afrika Kusini ni "nchi yenye vurugu nyingi".



Kwa mfano, alieleza kuwa mauaji yameongezeka kwa karibu 21% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.



Linapokuja suala la unyanyasaji wa kijinsia, alisema kuwa watu 9,500 walibakwa katika muda wa miezi mitatu - sawa na ubakaji wa watu nne kwa saa.



Hilo ni ongezeko la 7% kutoka mwaka jana.



"Mengi zaidi yanaweza kutokea, lazima kuhakikisha kwamba raia wa Afrika Kusini wako salama na wanahisi kuwa salama," Bw Cele alisema.



Lakini aliongeza kuwa wakati takwimu zikiwa bado mbaya kuna dalili kwamba mambo yanaendelea vyema.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad