Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi ya Tuvalu, Simon Kofe ametoa hotuba kwenye Mkutano wa 26 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi #COP26 unaofanyika Mji wa Glasgow, Scotland, akiwa amesimama ndani ya maji ya Bahari ili kuonesha jinsi Nchi hiyo ilivyo mstari wa mbele katika mapambano ya Mabadiliko ya Tabianchi .
Picha za Kofe akiwa amevalia suti na tai huku akiwa ameikunja suruali yake hadi magotini huku akitoa hotuba hiyo ambayo imerekodiwa na kuoneshwa kwenye Mkutano huo, zimegusa hisia za Watu wengi mtandaoni.
“Nimetoa hotuba nikiwa ndani ya maji ili kuonesha uhalisia wa maisha halisi tunayopitia Watu wa Tuvalu ikiwemo kuathirika na mabadiliko ya Tabianchi kunakosababisha kuongezeka kwa kina cha maji ya Bahari na kutishia Usalama wa Wananchi wa Tuvalu hasa ukizingatia kuwa tupo Visiwani lakini pia nimeelezea hatua tunazochukua kutunza mazingira” Kofe