Waziri Aweso asema maji Dar bado hali si shwari





Ikiwa zimepita siku 15 tangu Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) kutangaza mgawo wa maji, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema hali bado si shwari.


Aweso ametoa kauli hiyo leo alipotembelea mradi wa visima saba wa Kimbiji ambao unatarajiwa kumaliza changamoto ya maji katika wilaya ya Kigamboni.



Waziri huyo ameeleza kuwa licha ya jitihada zinazoendelea kufanyika kwa kuwaondoa wanaochepusha maji kwenye mto Ruvu bado maji yanayoshuka si kama ilivyokuwa hapo awali hivyo amewataka wakazi wa jiji hilo kuwa na matumizi mazuri ya maji yanayopatikana.



“Mara ya kwanza mtambo wa Ruvu chini pampu zetu zilikuwa hazifanyi kazi kwa sababu maji yalikuwa chini kabisa, bado hatuko stable….



“Baada ya kufanyika zile operesheni za kuwaondoa wachepusha maji, zimesaidia yale maji kuingia kwenye mkondo wa mto Ruvu na kutupa nguvu kidogo kwa maana zile pampu ziweze kujiendesha ili watu waweze kupata huduma ya maji.



Amesema, “Kwahiyo bado nasisitiza hatuko stable ndiyo maana nasisitiza wananchi kile kidogo tunachokizalisha kinatumika vizuri na tunakihifadhi ili tuweze kuvuka salama,”.



Waziri Aweso pia amewataka Dawasa kuhakikisha ratiba za mgao zinazingatiwa na zinawekwa wazi kuhakikisha wakazi wote wa Dar wanapata maji.



“Utaratibu wa ugawaji maji uwe wazi, kama jumatatu wanapata maji Kigamboni basi wapate, kama Jumanne Sinza iwe hivyo.



“Kingine niwaombe Dawasa visima vyote vilivyochimbwa pembezoni na katikati ya mji viwe standby, vijulikane ili tujipange zaidi vituwezeshe kuvuka salama,” amesema Aweso.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad