Waziri Bashungwa awaagiza BASATA kumsaidia Mzee Stima

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lishirikiane na Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania,(CHAMUDATA) kumpeleka hospitali  mwanamuziki mkongwe,  Mzee Hussein Abdallah Stima mwenye umri wa miaka 85 anayesumbuliwa na maradhi ya moyo na presha tangu mwaka 2020 ili aweze kupata matibabu mara moja.


Mhe. Bashungwa ametoa agizo hilo leo Jumanne (Novemba 30) alipomtembelea Mzee Stima nyumbani kwake Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam kumjulia hali.


“Fanyeni taratibu zote zinazohitajika haraka ili mzee wetu apatiwe matibabu, hili linawezekana”. alisisitiza  Mhe. Bashungwa.


Katika hatua nyingine Mzee Stima ametoa wito kwa wasanii kuimba nyimbo zinazohamasisha maendeleo ya taifa na uzalendo kwa nchi yetu.


Mzee Stima ni miongoni mwa wanamuziki nguli nchini anayejulikana  kwa umaridadi wake wa kupuliza Tarumbeta (Saxophone) uliowakosha watu wengi ikiwa ni pamoja na  hayati  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Enzi za ujana wake Mzee Stima amefanya kazi katika bendi mbalimbali ikiwa ni pamojana na Cuban Marimba, JWTZ Mwenge Jazz, Vijana Jazz, S.A. Rhumba na  Washirika Njatanjata.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad