Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwa sasa anaripotiwa kuwa mstari wa mbele na jeshi la nchi yake akikabiliana na waasi wa Tigray katika mkoa wa Afar.
Habari hiyo ni kwa mujibu wa kituo cha televisheni chenye kuegemea upande wa serikali cha Fana. Katika taarifa hiyo ambayo imeshindwa kuthibitishwa na shirika la habari la Uingereza Reuters, Abiy anaelezwa kuonekana akiwa kavaa magwanda ya kijeshi na kuzungumza kwa lugha ya Kioromo na Amharic Abiy aliyevaa kofia na miwani ya jua anatajwa kusikia akionesha mlima ulikuwa mbele yao kwa wakati huo na kusema ulikuwa umetekwa na maadui hadi jana. Lakini kwa sasa wamefanikiwa kuudhibiti.
Aidha kiongozi huyo aliongeza kusema hawatarejea nyuma mpaka wahakikishe ushindi na uhuru wa Ethiopia.Jioni ya Jumatatu kiongozi huyo alitangaza atakwenda katika uwanja wa mapambano kuongoza mapigano dhidi ya wapiganaji wa eneo la kaskazini la Tigray na washirika wao.