Waziri mkuu wa Iraq anasurika kuuwawa kwa ndege isiyorushwa na rubani




Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al-Kadhimi, amenusurika katika jairibio la mauaji kwa shambulizi la ndege inayorushwa bila ya rubani. Taarifa hiyo ya leo ni kwa mujibu wa jeshi la nchi hiyo.


Likinukuu chanzo cha habari cha kijeshi, shirika la habari la serikali ya nchi hiyo, INA, limesema shambulizi lililenga makaazi ya al-Kadhimi, ambayo yapo katika eneo mashuhuri liitwalo Ukanda wa Kijani, mjini Baghdad.



Muda mfupi baada ya tukio hilo lililoshindwa, waziri mkuu huyo alijitokeza kwa kusema anaendelea vyema na kutowa wito wa utulivu na watu kuwa wavumilivu. 



Shambulizi hilo linafanyika katika kipindi ambacho Iraq imegubikwa na maandamano dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa bunge wa mwezi uliopita ambao makundi yenye kuiunga mkono Iran yalishindwa vibaya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad