Waziri mkuu wa Sudan aliyerejeshwa madarakani Abdalla Hamdok, Jumanne ameiambia televisheni inayoendeshwa na serekali ya Saudi Arabia, ya Al Arabiya kwamba amelitaka jeshi kumaliza ghasia dhidi ya waandamanaji. Hatua ya jeshi kuchukua madaraka Oktoba 25 kumesababisha maandamano, na vuguvugu la chama cha madaktari ambalo limeungana na waandamanaji ambapo limeeleza kwamba vikosi vya usalama vimeuwa raia 41 na limeongeza ghasia za kusaka watu. Pamoja na maelezo hayo ya waziri mkuu Hamdok, ameongeza kusema kwamba anatarajia serekali mpya itaundwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo. Awali waandamanaji na vyama vya siasa vilivyokuwa vikipinga maandamano vilieleza kutofursahishwa na hatua ya waziri mkuu Hamdok kuingia katika makubaliano na jeshi.