Will Smith Atamani Kujiua





Mshindi wa Tuzo za Grammy na muigizaji wa Kimarekani, Will Smith amezua mjadala mitandaoni baada ya kutamka kuwa kuna wakati alitamani kujiua.

Hayo aliyasema kupitia tangazo la kipindi chake kipya kitakachorushwa YouTube Novemba 8, kinachoitwa ‘Will Smith: The Shape of My Life’, Smith katika tangazo hilo fupi anaonekana akiwa amekaa na familiya yake na kuwaambia juu ya namna alivyotamani kujiua.

Sababu za kutaka kujiua bado hajaziweka wazi, Smith atakuja na kipindi chake kutokana na  kunenepa ghafla tangu Marekani waweke zuio la kutoka majumbani  (Lockdown)  kufuatia mripuko wa virusi vya Corona, hali iliyopeleka Smith kuwa mnene kuliko kawaida.  

Smith kupitia kipindi hicho ataonesha jinsi alivyopunguza 9 kg kwa muda wa wiki 20 huku akieleza upande mwingine wa maisha yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad