Huwezi kuona thamani ya kitu mpaka siku ukikose!
Wako wapi wasanii wale waliopiga kelele kuwa wanashindwa kung'ara kwakuwa marehemu Ruge alikuwa anawanyonya? Wengi nawaona wakiwa na hali mbaya kuliko hata kipindi cha kunyonywa na marehemu.
Leo sitajadili uwezo na vipawa vya Ruge kwenye tasnia nzima ya mziki wa kisasa lakini kuna siku historia itampa heshima anayostahili...Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kama hujui basi katika kundi ambalo halina shukrani wala fadhila basi ni hili kundi la wasanii wa kibongo, wote wa mziki na maigizo kwa mukatadha wa mada hii
Hulka sugu ya hawa watu ni ile dhana ya kupenda kitonga kwenye kila kitu.. Utamtoa jalalani uswekeni akiwa ni kapuku asiye na mbele wala nyuma utatumia gharama kubwa kumbrand na kumng'arisha... Akishang'aa na kuonekana mtu kati ya watu, thamani yako inakomea hapo
Atasahau kila kitu
Atasahau namna ulivyomfadhili
Sehemu ya kulala
Mavazi na mapambo
Chakula na vinywa
Usafiri
Gharama za studio
Matumizi ya kila siku nknk
Ole wako...nasema ole wako akishakuwa maarufu uje umkumbushe ulikomtoa ama ujaribu kumshauri kitu.. Utajuta kumfahamu
Sakata la Harmonise na lundo la tuhuma kwa Diamond limenikumbusha mengi lakini pia limefunua na kufumua mengi...Hakuna ubishi Harmonize ni msanii mzuri mwenye kipaji cha utunzi na uimbaji na ni mpambanaji asiyekata tamaa..kushindwa kuliona hili ni wivu mbaya kabisa.. Lakini kinachomsumbua ni vitu viwili vitatu
Hulka
Elimu/ uzoefu
Wapambe/makundi
Hulka ya kulalamika na kutaka kuona kaonewa sana, hili linatokana na kukosa uzoefu wa maisha unaotaka na elimu haba toka kuhitimu mpaka ajira
Wapambe na makundi.. Hawa ndio wanaweza kuwa kaburi lake kisanaa.
Ni kati ya hawa bila kumpamba pamba kwa maneno mazuri na matamu wanaona kula yao iko hatarini.Hawa ndio chawa wenye kutunga kila aina ya uzushi
Kuna makundi ya washindwa.. Hawa ni haters wa Diamond , wamo wasanii na wasio wasanii, hawa wanamtumia Harmo kutolea hasira zao kwa Mond..Yaani wanaona kushindwa kwao kumesababishwa na Mond
Hawa si kwamba wanampenda na kumjali sana Harmo la hasha wako naye hapo kutaka kupata kula yao lakini pia kutaka kumdidima Mond.. Ni kundi lenye wivu na roho mbaya sana na ni kati yao hao watakaokuja kumgeuka Harmo atakapofanya vizuri zaidi.. Ni kundi hili ndio lilikuwa mstari wa mbele kumsema marehemu Ruge leo limemgeukia Mond
Udhaifu wa mikataba upo popote pale duniani.. Labda pengine Harmo halifahamu hili..kupigwa kwenye mikataba ni jambo la kawaida sana, kama nchi na wasomi wake wote inabamizwa itakuwa yeye? Akumbuke hata lebo yake ya Konde boy kama ikisimama vema na kukua itakuja kukumbana na changamoto hizihizi anazozishikia bango kwa Mond
Ishu ya kusema kuwa alituhumiwa kutaka kumzidi boss wake hayo ni mambo ya kawaida sana mbona? Awaulize walio kwenye ajira hasa sekta binafsi ataambiwa.. Nguo nzuri kumzidi boss zinaweza kukuondoa kazini...
Je ya JK na Lowassa anayajua? Shetani mwenyewe alipoleta ujuaji na kutaka nafasi sawa na Mungu alipatiwa haki yake! Mond kafanya ni bjnadamu, Harmo naye atakuja kufanya.. Boss huwa anabaki kuwa boss kataa kubali!
Katuonesha mfanano wake na Musiba...Kumbe kule kujikomba kote kwa mwendazake ni kwa vile alisaidiwa madai yake! Akasahau kila kitu akajitia upofu mkubwa na kumbwagia kila aina ya sifa hata kama mamilioni walikuwa wanaumia..huu ni ubinafsi na choyo kikubwa
Ameshatapika ya kutosha sana, pengine ana nafuu sasa.. Lakini huu ndio muda wa kujitafakari zaidi.. Aliyemshambulia sana hajamjibu kabisa.. Hili linaumiza pia. Dunia tunayoishi ni ya survival of the fittest .. Ile ya upendo na huruma aliondoka nayo Kristo...Ishu ya kupata connection serikalini kupitia JP inamjengea maadui bila kujijua na wengine kati yao ni hao alionao sasa
Viatu vya Ruge bado vinatafuta mrithi