Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema mjadala ulioanzishwa na baadhi ya wachambuzi kuhusu udhamini wa Kampuni ya GSM kwa klabu mbalimbali Ligi Kuu Tanzania Bara ni siasa chafu kwa kuwa siyo jambo geni katika ulimwengu wa soka.
Injinia Hersi amesema: “Watu wanaleta siasa chafu na mimi nasema hizi ni takataka. Mbona kampuni kama Emirates inadhamini vilabu vingi tu vinacheza ‘Champions League’. Inamaana Arsenal wakicheza na AC Milan utasema mmoja amwachie mwenzake?” alihoji Eng. Hersi na kuongeza:
“Yanga inalipa mishahara yenyewe, ina mifumo yake ya kuajiri watu sisi tunasaidia tu. Yanga ni timu kubwa huwezi kufananisha na hawa makolo. Huwezi kumleta mchezaji kama Bangala halafu hajui mshahara analipwa na nani.
“Hii ni klabu kubwa, tunafanya kazi ya kurejesha heshima yake, watu waipende tena. Angalia mechi ya juzi Yanga inafungwa goli mashabiki wanapiga makofi, tunarudisha tunafunga la pili na la tatu na bado kuna dakika kama 900 za kucheza.”