Zijue sababu za kutokupungua wakati unafanya diet




Watu wengi wamekuwa wakikumbana na hili tatizo la kufanya diet lakini bado wakirudi kupima uzito kwenye mizani mambo huwa ni yale yale au hata kuwa mabaya zaidi.

Makala ya leo itakuonyesha juu ya ulaji ulio wa afya na pia ulio sahihi kukusaidia kupunguza uzito wako.

Kutoruka mlo wa asubuhi (breakfast)
Wengi wetu tumejikuta tukimaintain kwa kuruka breakfast na baadae kujikuta tukifidia ule mlo kwa kula chakula hata kingi zaidi

Muda wa kula
Muda mzuri wa kula ni masaa manne baada ya kuamka, mchana na masaa takribani matatu kabla ya kulala,hii huupa mwili wako mda wa kukimen’genya chakula vizuri na kuyeyusha mafuta yaliyopo kwenye chakula

Aina ya chakula
Aina ya vyakula sahihi tunavyopaswa kula ni vyakula vyenye protein kwa wingi,mboga za majani na matunda kwa wingi pia ,wanga kidogo bila kusahau unywaji maji ya kutosha.

Kutokuwa na msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo au stress hupelekea kula vyakula ambavyo sio sahihi kwa afya yako na kwa wingi kama vile pombe, snacks mfano crips, biskuti, pipi, chocolate na kadhalika hata hivyo mwili huhifadhi mafuta kwa wingi kipindi ukiwa na stress.

Kupata usingizi wa kutosha
Inashauriwa kulala masaa 6 hadi 8, kwani Kutopata usingizi wa kutosha hufanya mwili wako kumen’genya chakula taratibu.

Lakini pia diet tu haitoshi mazoezi nayo ni muhimu katika kupunguza uzito, hakikisha unafanya mazoezi walau mara tatu hadi nne kwa week kwa muda wa dakika 20 hadi 30

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad