JUMLA ya Timu 14, kati ya 16 zimefanikiwa kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, mara baada ya kushinda michezo yao ya mtoano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu….(endelea)
Michezo hiyo ya marudiano ilipigwa jana Jumapili, tarehe 5, Disemba 2021, katika viwanja mbalimbali.
Timu ya kwanza kufuzu katika hatua hiyo ilikuwa ni Simba ambao wal;ishuka dimbani mapema majira ya saa 10, ugenini kumenyana na Red Arrows ya nchini Zambia na kupoteza mchezo huo kwa mabao 2-1, lakini walifanikiwa kufuzu kutokana na kuwa uwiano mzuri wa mabao.
Simba ilifuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-2, katika michezo yote miwili, mchezo wa kwanza ulipigwa Dar es Salaam, tarehe 28, Novemba 2021 Simba ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-0.
Klabu zingine ambazo zimefuzu kwenye hatua hiyo ya makundi ni pamoja na As Otoho na TP Mazembe kutoka nchini Congo, Coton sport ya Cameroon, Asec Mimosas, Orlando pirates kutoka Afrika Kusini, US Gendarmerie ambao wamefuzu kwa mara ya kwanza.
Wengine ni Al Masry sc, Pyramids zote kutoka Misri, Zanaco ya Zambia, Js saoura, Cs Sfaxien kutokaTunisia, Ahly Tripoli ya Libya na RS Berkane kutoka nchini Morocco.