1: WHAT A MATCH🙌 WHAT A GAME... WOW.. JUST WOW.. Hii ndio DERBY YA KARIAKOO .. HII NDIO 'DERBY' BORA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI NA KATI✊ AFRIKA imetujuaa🔥
2: ASANTE FRANCO.. ASANTE NABI! Ubora wa Dakika 90 za Derby ulianzia kwenye mkoba wa mbinu zao.. Walisomana, walijuana na wakapeana maswali yaliozaa Burudani kubwa kwa mashabiki.. Asante sana 👏
3: Mechi ya wazi. Mechi ya kasi! Simba kwenye Formation ya 4-3-3 walifanikiwa sana kwenye kujua eneo sahihi la kumuanzisha Benard Morrison.. Kwenye 'Zone ya 14' kasi na Maarifa yake yalikuwa na swali gumu kwa Bangala na Aucho kuyajibu
4: Nabi kwenye 4-2-3-1 .. Alibakia kwenye system yake! Kama kuna mtu anaweza kumlaumu kwa kushindwa kutimiza jukumu lake kimbinu basi ni Ntibazonkiza! Kwanini?
5: Hakuwa na msaada muda Timu ilipokosa mpira! Lakini alikosa madhara pia muda ambao Yanga walikuwa na mpira.. A player with his quality alitakiwa kushinda zaidi 1v1 situation dhidi yake na Kapombe
6: KANOUTE.. ! Very Simple.. Ukipenda Mpira, Utampenda Kanoute. Mchezaji mwenye nidhamu kubwa ya kimbinu. Kwrnye 4-3-3- ya Simba alichagua kucheza upande wa kushoto! Lengo ni kumpa msaada Tshabalala kwa Moloko.. Alielewa mchezo, akacheza Kikubwa!
7: Kama kuna mahala Pablo alifanikiwa sana mbele ya Nabi ni kuukataa ule mtego wa Yanga kwenye 'Build Up'! Ukiwa huna wachezaji sahihi na ukachagua Highline Pressing kwa Yanga.. Umekwisha! Simba walijua udhaifu wao wakarudi kwenye Mid Block! Yanga wakakosa Plan B
8: ASANTE ONYANGO👏 ASANTE VARANE! Mabeki wakubwa kwenye mechi kubwa. Walisoma vyema ubora wa Mayele na wakajua jinsi ya kudili nae kwenye udhaifu wake.. What A Perfomance kwa Ukuta wa Simba! Asante sana Tshabalala kwa nidhamu ya eneo
9: Elly Sasi! Alipata nafasi ya kuchezesha mechi bora sana ya Derby.. Bahati mbaya kwake, ameacha kumbukumbu matukio yasiokuwa na majibu! Why alistopisha shambulizi la Simba kwenye eneo la Hatari? Yeye anajua zaidi
10: Ukuta wa Yanga.. 🙌 Wow! Kibwana Shomari.. Dickson Job.. Mwamnyeto! Wanastahili heshima kubwa vijana wale. Walicheza kwa kikubwa.. Ubora wa kusoma mchezo na kufanya Timing nzuri kwenye kupokonya mipira👏
Nb: Wamshukuru Refa ... 😃