SIM Card (laini za simu) ni moja kati ya mfumo ambao umebakiza maisha mafupi katika teknolojia. Kampuni nyingi za kutengeneza simu zinaelekea kutoa sehemu ya kuweka line ya simu na kuhamia katika mfumo wa “embedded-SIM (eSIM)”, au “embedded universal integrated circuit card (eUICC)”.
eSIM ni mfumo mpya ambao unawezesha watumiaji wa simu kuunganisha namba ya simu na mtandao wa simu kwa njia ya kielektroniki. Kila simu itakuwa na uwezo wa kuunganisha namba ya simu na mtandao bila kulazimika kuweka SIM Card (Laini ya Simu).
Hivi karibuni, Apple imetoa taarifa kwa mitandao ya simu nchini Marekani kuwa September 2022 itaanza kutoa simu ambazo hazitakuwa na sehemu ya kuweka SIM Card.
Tayari iPhone 13 zote zina uwezo wa kuunganisha eSIM na unaweza kutumia bila kuweka SIM Card, na kuanzia robo ya pili ya mwaka 2022 Apple itaanza kutoa iPhone 13 ambazo hazitakuwa na sehemu ya kuweka line.
Tayari Apple imeanza kuweka iPhone 13 ambazo hazina sehemu ya kuweka SIM card katika Apple Store na Apple.com.
Apple itatoa sehemu ya SIM Card kwa baadhi ya iPhone katika baadhi ya maeneo (masoko ya simu). Mwaka 2022 zipo iPhone 14 ambazo zitakuwa na sehemu ya kuweka SIM Card lakini iPhone za mwaka 2023 zote zitaacha rasmi mfumo wa kutumia SIM Card na kuhamia katika mfumo wa eSIM.
Cc @itsapolloo