Barbara wa Simba Ataangushiwa Kitu Kizito Hivi Karibuni



Na @johnharamba
Soka ni mchezo wa kihuni, ndiyo! Ni mchezo wa kihuni, iwe ni kwa kificho au wazi.

Kuanzia uwanjani, kuna uhuni mwingi tu unaofanywa na wachezaji, mfano faulo za siri (japo siku hizi teknolojia imechangia kupunguza faulo hizo), lugha za kukera (hii hata waamuzi wanatoa lugha hizi, ukimjibu anakulima kadi ukafie mbele ya safari).

Ukirudi nyuma uswahilini au mtaani ambapo ndipo kwenye chimbuko la soka kuna wahuni wengi tu wanafanya kweli kisoka, na hao ndiyo ambao wengi wanafanikiwa au wanakuwa wachezaji wakubwa duniani.

Siyo tu Tanzania bali duniani kote asilimia kubwa ya watoto waliotokea mtaani wamefanya vizuri kuliko wale wa kishua ambao wanategemea kukuzwa na mbinu za akademi.

Upande wa pili hata viongozi wanafanya uhuni mwingi tu iwe ni katika usajili au katika ushindani wa maslahi.

Unakumbuka Sepp Blatter alivyokuwa mfalme wa soka duniani! Kilichomtokea ule ni sehemu ya uhuni, alisetiwa akajaa akatumbuliwa.

Mifano ipo mingi kuna viongozi wengi hapa Tanzania, wamewahi kulipwa faini, kufungiwa na hata kupotezwa katika soka mazima kwa kuwa tu waligusa maslahi ya watu wenye mamlaka au ya taasisi yenye nguvu, hivyo wakawa hatarishi kwa maslahi ya kina fulani.

Hivi karibuni Bodi ya Ligi ilitangaza kusaini mkataba na GSM Group wenye thamani ya Sh bilioni 2.1 kwa miaka miwili.

Simba kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji, Barbara Gonzalez wakawa mstari wa mbele kupinga mkataba huo kwa sababu walizozieleza wao, pia wakagoma kuweka nembo ya GSM kwenye jezi zao.

Bodi ya Ligi wakaweka mabango yenye nembo ya GSM uwanjani katikabenchi la Simba, Msimbazi wakaweka ngumu, kwelie mabango yakatolewa, hiyo inamaanisha wazi walikuwa na hoja wamewashinda nguvu ya hoja Bodi kwa hoja.

Kwa uhuni wa soka ninaoujua, hilo halitapita hivihivi.

Jumamosi hii tena, Barbara akazuiwa kuingia uwanjani, akaishutumu Bodi, baadaye TFF ikatoa tamko la kumshutumu Barbara na viongozi wenzake kadhaa wakati wa kuingia uwanjani.

Kwa aina ya utamu wa soka ulivyo, inawezekana hivi karibuni ‘uhuni’ nilioutaja hapo juu ukasababisha bibie adondokewe na kitu kizito.

Source : @timesfmtz
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad