Muimbaji wa Marekani, Billie Eilish amesema kutazama video za ngono mtandaoni kuliharibu ubongo wake kwakuwa alianza kuzitazama ingali akiwa mdogo.
Billie ambaye kwa sasa ana miaka 19 amesema hayo Jumatatu wakati akihojiwa kwenye The Howard Stern Show.
“Kama mwanamke, nadhani video za ngono ni aibu,” alisema kwenye mahojiano hayo. “Nilikuwa naziangalia sana, kusema ukweli. Nilianza kuangalia pindi nina miaka 11.”
Aliendelea,” Nadhani ziliharibu kabisa ubongo wangu na najihisi kuvunjika kabisa kuwa niliangalia sana.”
Amekiri kuwa ilifika wakati alikuwa akiangalia video zenye vitendo vya kutisha na kikatili zaidi.
“Nilikuwa bikira. Nilikuwa sijafanya chochote. Na pia ilinipelekea kwenye matatizo.
Mara ya kwanza nafanya mapenzi nilikuwa sikatai vitu ambavyo havikuwa vizuri. Kwasababu nilidhani hivyo ndivyo nilipaswa kuvutiwa navyo,” alisisitiza.
“Nina hasira sana kuwa video hizo zinapendwa. Na nina hasira kwangu mwenyewe kwa kudhani ilikuwa sawa.”
Muimbaji huyo amekiri kuwa zilimfanya kuwa na fikira zenye kasoro kuhusu tendo la ndoa na mahusiano.