Reposted from @shaffihdauda_ Wakati Metacha Mnata anaondoka ndani ya Yanga Kuna vitu huenda Viongozi walivisahau au huenda walifumba macho kwa kujua au kutokujua
Metacha alikuwa Golikipa namba mbili nchini nyuma ya Aishi Manula, unamuachaje aondoke kirahisi?? Golikipa mwenye umri mdogo na ubora anao
Ila wakampa Mbwa jina baya Ili wampige mawe, ila nyuma ya pazia ilikuwa kisa vita ya Meneja wake @jemedarisaid ambaye yeye ana misimamo yake ambayo baadhi ya Watu ndani ya Yanga wanaiona kama kinzani
Wakaamua kumuondosha Kijana Mdogo kisa vitu personal vya Meneja wake, wakihisi wanamkomoa Mchezaji lakini haikuwa hivyo na Wala haikupaswa kuwa hivyo
Leo hii Kocha anamtazama Metacha kama backup sahihi ndani ya Jangwani, kwa kushinikiza baadhi ya Watu ndani ya Yanga, mkashinikiza Kijana abwagane na Meneja wake tena mtandaoni
To me naona huo sio weledi, Jemedari yeye ana mtazamo wake ambao unapaswa kuheshimiwa, hatuwezi wote kufikiria sawa na kuwa na mawazo yaliofanana, zaidi hamumkomoi yeye kidogo zaidi ni kutaka kuharibu reputation yake tu
Kwahiyo mkipishana na Mtu kimawazo ni lazma vitu binafsi vihusu Taasisi? That's immaturity kwa baadhi ya Watu klabuni
Kwahiyo zile tuhuma za 'kupachikwa' zinafutwa vipi?